Kama hujasoma vitabu hivi basi wewe umekosa utamu wa kusoma vitabu

Kama hujasoma vitabu hivi basi wewe umekosa utamu wa kusoma vitabu

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,697
Katika nyumba vitu vinavyoibiwa sana na watu wako wa karibu kabisa ni vitabu, kama una shelf ya vitabu kaa mwaka mwaka mmoja halafu ukaikague shelf yako lazima utakuta robo tatu ya vitabu vyako vimeibiwa.
sababu kubwa ya wizi huo ni raha iliyomo katika hivyo vitabu.

Kwa masikitiko makubwa shelvu yangu imeibiwa vitabu vifuatavyo ambavyo kama hujavisoma basi umekosa raha ya kusoma vitabu:-

1. Mossad (watunzi ni Eli Randau, Denis Essenberg na Uli Dani) ni kitabu kinachohusu shghuri za ujasusi la Israel.
2. In GOD` s Name by David Yallop hiki kinahusu kifo cha Papa John Paul wa 1 yule aliyedumu madarakani mwaka mmoja tu.
3. The LUST to KILL by David Kyemba kinahusu mauwaji ndani ya utawala wa Idd Amin yule aliyempindua Obote na kufurushwa madarakani na Majeshi ya Tanzania
4. General Amin mtunzi kidogo nimemsahau
5. Carlos the jACKAL kinahusu yule terrolist aliyesumbua ulaya miaka ya sabini ikiwemo na utekaji wa wana michezo wa Israel katika michezo ya Olympic huko Munich mwaka 1972.
6. Entebbe Raid kinahusu kikosi cha Makomandoo cha jeshi la Israel kilichofaulu kuwaokoa mateka wa kiyahudi walotekwa kwenye ndege abiria ya Ufaransa na kuhifadhiwa Entebbe wakisubiri madai yao yatekerezwe na nchi ya Israel kabla ya utekerezaji huo mateke wakaokolewa usiku, Idd Amin akabaki anabung`aa tu.

Vitabu vyote hivyo vinahusu matukio yaliyotokea kweli duniani.

Yoyote mwenye kitabu cha MOSSAD ani PM nitakinunua kwa bei yoyote
 
Mbona documentaries zipo nyingi you tube kuhusu operations za Mossad
 
Kati ya kazi ambayo hainiingizii hata kumi kwenye maisha yangu ni kusoma hayo mavitabu bora niwaze ntapataje hela kuliko kusoma mawazo ya watu tena yasiyokuwa na mchango wowote kwenye mazingira ninayoishi ni nimeshindwa kwakweli
 
Mimi uwa naficha pesa kwenye vitabu hakuna anayeziona! wengi mawazo yao ni kama yako.
 
Kati ya kazi ambayo hainiingizii hata kumi kwenye maisha yangu ni kusoma hayo mavitabu bora niwaze ntapataje hela kuliko kusoma mawazo ya watu tena yasiyokuwa na mchango wowote kwenye mazingira ninayoishi ni nimeshindwa kwakweli
Yaani wewe husomagi vitabu, yesu wangu, sasa watoto wako huwa unawaambia nini? wakawe wezi stand?
 
Njoo PM

Adjustments.JPG

View attachment 1537413

View attachment 1537414

View attachment 1537415
 
Back
Top Bottom