Kama hujui lugha za kigeni, umechelewa game – Wajua wenzio wanahit cash kwa kuongea tu?

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Wadau wa JamiiForums,

Ngoja niwanyooshee huu uzi straight kama line ya sare za jeshini, maana watu wengi bado hawajastuka kuwa lugha za kigeni ni life-changer. Si mapambo ya CV, si mbwembwe za kujionesha Instagram, ni fursa halisi za kutokea mitaa hadi ulaya bila hata passport kuvuja jasho.

Mimi ni tour guide, na napiga French (Kifaransa) na German (Kijerumani) kama kawaida. Hizi lugha zimenibadilishia game, zimenitoa kule mtaani ambako tulikuwa tunasikilizia Wi-Fi ya jirani, hadi kwenye meza za kimataifa ambako unazungumza na mzungu unamwelewa live bila Google Translate.

Sasa ngoja nikuweke straight – Hizi Ndio Real Talk Za Mtaa na Dunia Ya Kisaasa:

1. Ukijua lugha ya watu, unakula nao bila invitation.
Hii dunia haikusubiri bro – ukiwa na Kiswahili tu, ni kama kuwa na gari bila mafuta. Lugha ya pili ni kama turbo. Ukiwa na ya tatu – damn, you a beast in the hustle game.

2. Lugha ni kama silaha – unaingia sokoni bila stress.
Watu wanalipwa kwa kutafsiri, kuongea, kufundisha lugha tu online. Kuna vijana wanapiga $10 kwa saa kwa kufundisha French au Spanish Zoom. Wewe bado unakaa tu unapost status za “Natafuta kazi yoyote”.

3. Kama huna lugha, unacheza game bila controller.
Hakuna fursa ya kimataifa bila lugha. Mashirika ya UN, Red Cross, embassies, hata makampuni ya tours – wanauliza, “Do you speak another language?” Ukijibu no – it’s game over.

4. Ni hustle ya kihalali – no stress na police, no kubanana mtaani.
Jifunze lugha, fungua channel ya YouTube, fundisha watoto online, translate subtitles, toa tours, write CVs, do interpretation – yani uwanja ni mkubwa kama uwanja wa Taifa.

Kisomi Kidogo:

Lugha ni daraja la maarifa. Unapojua lugha ya kigeni unaelewa utamaduni, historia na fikra za watu hao. Unaweza kusoma vitabu vyao original, kuwasiliana bila barriers, na kuaminika kwenye jamii ya kimataifa. Unaenda kutoka "local man" hadi "global don".

Real Talk Ya Mwisho:

Mimi niliamua kujifunza lugha mtaani kwa simu ndogo tu, nikaanza na Duolingo, nikatafuta marafiki online – sasa hivi nazungumza na wazungu, napeleka watalii safari, nalipwa vizuri – life sweet. Hii yote ni kwa sababu ya lugha.

Kama mimi niliweza, wewe pia unaweza. Acha kubweteka, dunia haitakusubiri. Jifunze lugha, jiongeze, catch the bag.

Ukihitaji direction, niambie – nitakupatia njia ya kuanza hata leo.
 
Una hangaika Sana, humu jf ali kuwemo kontawa ontario kabla yako.

Hivi Kama nina kula na kushiba, Kuna haja gani ya kuhangaika ili kulipisha wengine ili wale Kama mimi?
Aaah! Kaka nimeachana na mambo za kulipisha kaka, saivi kila kitu ni bure tu maana nilinyooshwa humu sitokaa nlisahau kabisa kaka!
 
Umesema ukweli kabisa.ukijua lugha za kigeni ambazo zinazungumzwa na watu wengi duniani kama kiingereza,kifaransa au kichina hautahangaika sana kupata pakukuingizia kipato.Kuna wapuuzi wengi wanakuwa wanahamasisha watu kusoma kayumba ambazo hazina walimu na hawajui lugha za kimataifa na matokeo yake wanakuwa hawafahamu lugha muhimu na kuishia kuwa ombaomba mamia Kwa mamia kama wa pale ubungo interchange Dar es salaam
 
Merçi beaucoup. Ces sont sais francais, ils ont travaillent dans la plus metiers.

Makosa yako yapo hapa 👇🏽👇🏽
1. “Ces sont” inapaswa kuwa “Ce sont” — maana yake ni "Hawa ni..."

2. “sais francais” ni makosa ya tahajia. Unamaanisha “des Français” — "Wafaransa"

3. “ils ont travaillent” haiko sahihi. Ni mchanganyiko wa vifungu viwili: “ils travaillent” (wanafanya kazi) au “ils ont travaillé” (wamefanya kazi)

4. “la plus metiers” haieleweki kisarufi. Inaonekana unamaanisha “fani nyingi” — kwa Kifaransa ni “beaucoup de métiers” au “plusieurs métiers”

Sentensi sahihi 👇🏽
“Ce sont des Français, ils travaillent dans plusieurs métiers.”

Tafsiri kwa Kiswahili 👇🏽
Hawa ni Wafaransa, wanafanya kazi katika fani mbalimbali.
 
Ni kweli kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…