Kama Humphrey Polepole atabahatika kukutana na Ben Saanane na Mdude Nyagali naomba awambie yafuatayo

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709


Kama Humphrey Hezron Polepole atafanikiwa kuonana akina Ben Saanane na Mdude Nyagali naomba awambie yafuatayo;

Mosi, kabla hujafa hujaumbika.

Pili, mambo yanabadilika.

Tatu, aliyeko juu mngoje chini au mpandie.

Nne, aishie kwa upanga, atakufa kwa upanga.

Tano, atekaji unaendelea.

Sita, Lissu bado anadunda japo yuko lupango.

Saba, mgombea wa CCM alijiteua kugombea urais.

Nane, CCM sasa wanakulana wao kwa wao.

Hivyo, wasimshangae kuwa nao tena kwa njia ile ile.

Baada ya hapo, wamtafuta Jiwe na kumpa salamu za mtu wake aliyetengeneza na namna anavyoyabomoa mema aliyotenda kama kubinafsisha bandari huku akidumisha mabaya hasa utekaji. Pia, asisahau kumpa hii Azory Gwanda na wahanga wengine. Najua Polepole anawakumbuka sana.

Nafikiri na kuwaza kimya kimya.
 
Ujinga tu umeandika
Heri mie kuandika ujinga kuliko wewe kujibu ukumbaff mwanangu. Kwa wasio na kumbukumbu, Polepole ni shujaa. Kwa wahanga wa mauaji na utekaji na uuaji wa chama chake kipenzi, kinachompata ni malipo au mavuno ya kile alichopanda. Kuna ubaya gani macc wakiumbuana, kutekana na kuuana. Vita ya kunguru ni neema kwa panzi ati. Ugomvi baina ya maccm ni unafuu kwa wadanganyika.
 


Watz ni nyumbu wapumbavu nyie mnalalamika na I'd fake

Njooni uwanjani tupambane
 
Kinachonikisitisha humu ilitaki kuwe na uzi zenye misimamo kana kwamba tupo salama, nani alihisi watamdhuru ccm mwenzao Polepole? Tulizoea wapinzani na wengine.

Ila sisi humu tumejisahau hadi tunaleta mzaa mzaa kama vile tupo salama, watatufuata humu mmoja mmoja.

Watanzania wenzangu tubadilike tuwe na sauti moja ya kitaifa
 
Watz ni nyumbu wapumbavu nyie mnalalamika na I'd fake

Njooni uwanjani tupambane
Hili taifa liko divided tena kwa vijisababu vya kipuuzi sana, kwakweli hata huo ukombozi tusahau kwa hivi karibuni..

Imagine sasa hivi watu wanaojinasibu wanataka ukombozi eti wako bize wana rejoice yaliyomkuta Polepole na kuipongeza serikali ya samia? Sasa ni akili hiyo?

Sasa mtu kama huyu anaweza vipi kuungana na wafuasi wa Polepole katika kukamilisha hiyo mission nzima iliyopo mbele yetu?

Nimepia kule kwa Mange kwenye comments sections watu ambao wanasema october wanatoka wako wanaparuana kuhusu hili jambo lilimkuta HP wengine wakionesha kufurahishwa kwa sababu ya past yake na wengine wakijawa na hasira, sasa hapo kuna jambo lolote litafanyika kweli?
 
Watanzania wote ni makuma tu, woteeee ni keyboard warriors.
 
Mimi sikuyapenda matendo ya HP enzi za mwenda zake, na vile vile mimi siipendi ccm, na hakuna siku HP ametoka akaikana ccm,
basi kama haya yaliyomkuta yamemkuta akiwa ndani ya ccm hiyo ndo inaitwa mbwa kala mbwa, kama mbwa wameanza kulana wenyewe basi waache walane mpaka waishe, labda hiyo ndo itakua salama yetu sisi swala na kizazi chetu.
 
Mwaka 2016 Rais John Magufuli alimteua Polepole kuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma, mkoani Mara, alikohudumu kwa miezi michache kisha kuhamishiwa Ubungo Dar es Salaam kwa nafasi hiyo hiyo ya ukuu wa wilaya na kuhudumu kwa miezi michache pia.

Umaarufu wake uliongezeka alipoteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, nafasi ambayo kimsingi ni ya kuwa msemaji wa chama hicho kinachotawala Tanzania.

Anafahamika kwa kutetea sera na utendaji wa CCM na serikali ya Rais Magufuli, hata pale kulipokuwa na utata mkubwa wa masuala kama vile tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu, utekaji, kuwaweka watuhumiwa mahabusu kwa muda mrefu na wengine kufunguliwa kesi nzito za uhujumu uchumi na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020.
 
Mimi mmojawapo wa waliofurahishwa sana
 

Aisee 😳😳!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…