SoC02 Kama huna muda wa kusimamia miradi yako, bora ununue hata Bond za Serikali, kuliko kuteketeza pesa zako

SoC02 Kama huna muda wa kusimamia miradi yako, bora ununue hata Bond za Serikali, kuliko kuteketeza pesa zako

Stories of Change - 2022 Competition

ANAUPIGA MWINGI

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2022
Posts
389
Reaction score
757
Kwenye swala la kuhustle watanzania wengi tumekuwa na juhudi za kuanzisha kitu cha kando au biashara au miradi ya kando ili basi iweze kutusaidia kupambana na miasha ikisaidiwa na mshahara tunao pata. Wengi tumekuwa na biashara mbalimbali ikwemo Kilimo, Ufugaji, Maduka na kadhalika, Hii yote tumekuwa tunafanya ili basi itusaidie sisi na familia zetu.

Wengi wetu tumekuwa tunaanzisha biashara hizi na kuweka watu wasimamie, make sisi tunakuwa tumebanwa na majukumu ya kikazi, hivyo hujikuta ni lazima tuweke watu kama ndugu au kuajiri kabisa vijana na kuwaweka pale, hii hufanyika kwenye mashamba yetu, na hata kwenye miradi mingine kama maduka na kadhalika.

Mashambani mfano kule huwa tunajenga nyumba na kuepeleka vijana wa kazi, ambao hukaa kule kule na kuangalia mazao pamoja na mifugo, sisi sana huwa tunaenda mara moja moja siku za mwisho wa juma na kuna wakati hata mwezi unaisha bila kwenda kwenye miradi kwa sababu ya kubwanwa sana au kwa sababu ya kuona ni gharama sana kwenda mara kwa mara.

Hawa wasimamizi asilimia kubwa sio wasimamizi wazuri kwa sababu hata kama wangekuwa wazuri ila hawajui wazo lako na hawajui unako elekea wewe, hivyo mara nyingi tumejikuta tunakula hasara kubwa sana badala ya fadia na wengi huishia kufunga kambi kabisa na kurudisha mpira kwa kipa, kwa nini haifai kabisa kuwaacha waasimamizi wasimamie wazo lako au mroject yako?

Wizi mkubwa sana wanao ufanya- huu ni wizi wa mali zenyewe ambako mara nyingi hujikuta unapeleka vitu ambavyo kumbe mwisho wa siku vinauzwa, unapekeka dawa ya kuoshea mifugo yako kumbe vijana wanauza, unapeleka chakula cha mifugo kinauzwa, unapeleka ,mbolea zinauzwa, Dukani ni hivyo hivyo tena huko ndio nay eye huweka bidhaa zake, wewe unaona bidhaa haziendi kumhe nay eye kaleta zake anauzia humi humo. Hapa wewe mwenye wazo huikuta unakula hasara kubwa sana na mbaya unakuta umekopa pesa, umejinyima, watoto hata hawali vizuri ili uanzishe mradi ila matokeo yake yanakuwa sio.


MUDA-wanakuibia muda ukiachana na kukuibia mali, hawa unaweza ondoka na wao wakaondoka, kama ni duka wanaweza fungua hata saa 5, wewe unajua alifungua saa 12 kumbe kafungua saa 5, na anawez funga mapema anavyo taka, shambani ndio kabisa vijana wanaiba muda wanaenda kufanya kazi kwa wengine, yaani anakula bure ana lala bure bado anaacha mali zako zinaharibika ananda kufanya kazi kwa wengine.


Gharama kubwa za wewe kwenda kufuatilia,hapa inabidi uwe na gharama za kwenda mara kwa mara kuwafuatilia ili kuwasimamia au kuwaona wanafanya nini, na ukipotea mwezi siku unaenda unaweza lia, na wao hawana wasiwasi kabisa wanaona ni sawa na mbaya wanakuwa walisha andaa uongo wa kukueleza.


KUTO KUJUA MAWAZO YAKO-Wale wasiamizi hata kama angekuwa mjomba bado hawezi kuwa kama wewe, hajui unataka nini, hajui wewe unawaza nini, una ubunifu gani, vyote hivyo hajui.

Haya ndio yalifanya mimi ikabidi nika nao shambani na hata nikitoka ni masaa kadhaa narudi, watu wengi sana wamekuwa wanaibiwa, wamepata hasara kubwa sana, fikiria una project ya million 80 unamuchia kijana wa kazi, hii ni hatari sana. Huku Arusha kuna sehemu moja inaitwa kikwe niliwahi enda siku moja nikakuta kuna project moja ilikuwa ya Dada mmoja alikopa pesa benki jina la benki nalihifadhi, million zaidi ya 400 dada akawa amewekeza kwenye ufugaji, aliwekeza hasa miundombinu yote, fensi ya umeme, mabanda ya kuku, Ng’ombe, na nguruwe ni project kubwa sana ha ukifika ukaona kwa macho ilikuwa ni project hasa sio ya kitoto bali aliwekeza hasa. Makosa ya Dada yeye alikuwa anakaa mjini hivyo pale anakuja mara moja mmoja, kuangalia uzalishaji make walikuwa wanazalisha maziwa, wanauza mayai na Nguruwe pia, Dada mwenye idea alikuwa mjini vijana wasimamizi kama kawaida wakaanza kuhujumu, na aliweka hadi ndugu pale, huwezi amini projet ilifungwa na eneo likachukuliwa na benki sijui hata kama walisha uza au la.

Niliwaza sana nilivyo ona ile hali, na ule uwekezaji mkubwa vile na bado unaamua kukomaa kukaa mjini unaacha maliza million 400 kwa vijana wa kazi, nina mifano mingi sana ya hasara walizo [ata wadau kwa kuweka wasimamizi na wao kuwa busy na mambo mengine.

Muhimu ni nini?

Pesa inatafutwa kwa shida sana, hakuna kitu kibaya kama idea yako unawakabidhi watu wasio ijua waisimamie ni hatari sana,Idea yako inavyo kuwa changa au ndogo inakuhitaji sana wewe kuliko mtu mwingine yoyote Yule, ni sawa na mtoto mchanga anavyo hitaji sana maziwa ya mama kipindi cha mwanzo na akiyakosa basi anaweza pata shida sana huko mbeleeni.

Msimamizi mkuu wa wazo lako la biashara anapaswa kuwa wewe mwenyewe na wala sio mtu mwingine yoyote Yule, wewe ndo unajua unataka kufika wapi na wazo lako la biashara yako unayo fanya.Wengi tunazania kwaba suluhuisho ni kumuweka ndugu wa karibu hapana hio sio suluhisho hata huyo ndugu hawezi kuwa wewe.

Kama unakuwa huna muda na unapesa ni bora ukawekeza kwenye vitu ambayo havihitaji usimamizi kama vile kununua aridhi, kununua hisa au bondi za Serikali na pia kuwekeza labda kwenye miti, hivi vitu havihitaji usimamizi kabisa na pindi utakapo kuja kuwa na muda wa kusimamia basi unaweza fungu project zile ambazo unaweza zisimamamia sasa bila shida.Watu wengi sana wamekubwa na hili la usimamizi na kitu ambacho hawajakijua ni kwamba anaye takiwa kuwa msiamkizi namba moja ni Yule mweye wazo na wengine ndo wanafuata, kama mwenye wazo sio msimamizi namba moja basi

Wengine siku hizi wanashaurina kufunga Camera, utakacho zuia ni wizi ambao pia bado hao vijana wanaweza kuja na mbinu zingine, camera haiwezo tatua kila kitu hapo,Camera haiwezi fanya kazi za customer Care, haiwezi kuwa na idea za kuendeleza biahara yako, mimi huwa napinga sana kuweka Camera kwamba ndo iendeshe biashara hio ni makosa, weka kamera na wewe uwepo hapo.

Kwa kuhitimisha, ni kwamba usiwe unalalamika kwamba huna wasiamamzii, mara wasimamizi wanakuangusha sana, anaye paswa kuwa msimamizi wa kwanza ni wewe hapo na wale wengine ndio wafuate, wasiamizi wengine watafuata matendo yako na sio ushauri wako kwao, na ndo maana unaweza kuwa unaenda unaimba sana unawaelekeza sana ukiondoka siku ukirudi mambo ni yale yale,hii ni kwa sababu wewe unatoa sana ushauri badala ya kuwa mfano kwao.

Inaitwa telephone farming au telephone project, unaendesha project zako kwa simu.

Vipi kuku mmewapatia dwa?Mmeisha maliza kulima nitume mbegu? Muliweka dawa? Leo vipi wateja wamekuja?
 
Upvote 12
Interesting, ndiyo maana wahindi na wachina huleta watu toka kwao kuja kusimamia miradi yao. Watanzania tunaishia kulia ukosefu wa nafasi za juu za uongozi kwenye taasisi zao,,sisi sio waaminifu.
 
Nunua Bond, hisa kidogo kwa kampuni zinazofanya vizuri, nunua vipande UTT especially liquid fund au bond Bond Fund hapo Unapata passive income bila stress.
 
Kama huna muda wa usimamizi na una hela na unataka uizalishe..nunua vito vya thamani ikiwepo dhahabu..ama hifadhi hela zako katika us dola.

Pia nunua ardhi maeneo potential..ama jenga majumba ya kupangisha.
Ama weka utt amis ama bond za serikali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kama huna muda wa usimamizi na una hela na unataka uizalishe..nunua vito vya thamani ikiwepo dhahabu..ama hifadhi hela zako katika us dola.

Pia nunua ardhi maeneo potential..ama jenga majumba ya kupangisha.
Ama weka utt amis ama bond za serikali.

#MaendeleoHayanaChama
Yes, hii ni mbadala, ila kusimamia kwa simu ni kutafuta ugonjwa wa moyo bure
 
Interesting, ndiyo maana wahindi na wachina huleta watu toka kwao kuja kusimamia miradi yao. Watanzania tunaishia kulia ukosefu wa nafasi za juu za uongozi kwenye taasisi zao,,sisi sio waaminifu.
Tofauti yetu na wao ni kwamba wale wanajua Management, sisi tunakwama hapo, Watanzania unakuta sisi kwa sisi tunahujumiana, unaweza wafanyakazi badala wa kusaidie uinuke wanakuwa bide kukuhujumu
 
Maelekezo yako mkuu ni yenyewe. Ukweli mtupu. Bila usimamizi wa
karibu, project itaenda kaburini. Hata ujenzi bila kuwepo mwenyewe, siku ukienda site, hutaamini.
Watanzania ukiwapa muanya wana kumaliza, hawawazi kwamba huyu nduhu hebu tusimamie kazi zake na kadri anavyo pata ndio hivyo hivyo na sisi tutaneemeka, hilo hawawazi, wanawaza kukumaliza, kabisa
 
Back
Top Bottom