Kama jengo la Kariakoo ni miongoni ya yaliyosemwa kujengwa kinyume cha kanuni na Tume ya Lowassa, serikali ishitakiwe ili ifidie wahanga mabilioni!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Kamati iliyoteuliwa mwaka 2006 na Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa, ilibaini kuwa majengo 147 kati ya 505 yaliyokaguliwa jijini hayakuwa nyaraka na vibali sahihi vya ujenzi. Yalijengwa kiholela na bila viwango na kuwa hatarishi kwa uhai wa watu. Mnamo mwaka 2008, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliliambia Bunge kuwa kamati hiyo pia iligundua kuwa kanuni zilikiukwa kwenye ujenzi wa nyumba 81 huku wamiliki wa majengo 22 hawakufahamika.

Na sasa mmiliki wa jengo lililoporomoka inasemekana ni kiongozi serikalini, na huenda mwanasiasa. Kuna kila dalili kuwa serikali inamjua, lakini inamlinda, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Na tunajua, tangu wakati wa tume ya Lowasa hadi sasa serikali imeendelea kuwa ile ile ya CCM, ambayo ilipuuza ushauri wa watalaamu na leo hii inajiweka kimbelelembele na kuwa na unafiki wa kujifanya wamesikitishwa sana na tukio hili, na kusema itagharamia mazishi na vitu gani sijui kutokana na kuporomoka kwa jengo la Kariakoo.

Mimi naona serikali hii ya CCM inapaswa kupewa fundisho. Ndugu na jamaa wa wale waliofiwa na wale waliojeruhiwa katika tukio la Kariakoo, jikusanyeni muombe kusimamiwa na wanasheria, mkisaidiwa na TLS, muipige serikali hii kwa madai ambayo yataifanya ipate somo kwamba kiburi cha wanasiasa kujifanya wao ndio wanaojua kuliko wataalamu wetu kiishe. Msikubali hizo peremende za rambirambi, mnaweza kulipwa mabilioni kama fidia. Nendeni mahakamani mkadai fidia ya uhakika, kigezo kikiwa ni uzembe wa serikali katika kutekeleza ushauri huku ikijua imeonywa kuwepo kwa majengo hatarishi.

Ikiwa serikali ina uwezo wa kulipa mabilioni kutokana na uzembe wa kuvunja kisiasa mikataba na kampuni za nje, hata nyie mna uwezo wa kulipwa hayo mabilioni. Jiongezeni muishike hii serikali panapotakiwa!
 
Mtoa Uzi ahsante Kwa kuwajulisha wanasheria kuwa jengo la kariakoo kuporomoka ni fursa
 
Ni fursa nzuri ya kutoboa kimaisha, wengi wamepoteza wategemezi wao hasa waliokuwa wamepanga katika lile jengo. Kama serikali imeweza kulipa billion 72 chap chap kwa kampuni flani la kibeberu. Hawashindwi kuwalipa billion 50 wahanga wa ghorofa la Kariakoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…