PreGE2025 Kama Katiba yetu ya CCM inaruhusu Mageuzi (Reforms), Hao Wana CCM Wanaopinga Reforms kwenye Sheria zetu za Uchaguzi Nchini ni Wanachama wa CCM gani ?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Joined
Nov 15, 2019
Posts
49
Reaction score
128
Ndugu Watanzania, nianze kwa kuwasalimia kwa salamu ya chama changu pendwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kidumu Chama cha Mapinduzi ..........................!

Awali ya yote nitaomba radhi kwa kila Mwanachama wa CCM atakayekwazika kwa hiki ninachoenda kukifanyia uchambuzi.

SIKU ZA HIVI KARIBUNI kumeibuka vuguvugu la kisiasa nchini likidai Mabadiliko katika sheria zetu za uchaguzi likiongozwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huku ikiwa imesalia miezi michache kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Binafsi, kama kijana mzalendo wa nchi hii na Mwanachama Mtiifu wa CCM, NIMESIKITISHWA SANA na nguvu inayotumiwa na serikali yetu kwa kutumia vyombo vya dola kushinikiza mkwamo wa vuguvugu halali la wapinzani wetu kisiasa, vuguvugu linaloashiria matumaini mapya katika Uhuru kamilifu wa wananchi wa Tanzania, Maisha ya Watanzania kwa ujumla pamoja na Ukomavu wa Kidemokrasia nchini.

KWA MUJIBU WA Ibara 15 (2), (3) na (4) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Mwaka 2022, kila mwanachama ana wajibu wa ; -
(2) Kutumikia Nchi yake na watu wake wote kwa kutekeleza wajibu wake bila hofu, chuki wala upendeleo wa nafsi yake, rafiki au jamaa.

(3) Kujitolea nafsi yake kuondosha Umasikini, Ujinga, Maradhi na Dhuluma, na kwa jumla kushirikiana na wenzake wote katika kujenga Nchi yetu.

(4) Kuwa wakati wote mkweli, mwaminifu na raia mwema wa Tanzania.

Lakini vilevile, KWA MUJIBU WA Ibara ya 17 (2) na (3) ya Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la Mwaka 2022, Kiongozi wa CCM anatajwa kwa sifa ;-

(2) Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.

(3) Awe ni mtu anayependa kueneza matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwaajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

IKUBWE KUWA, WATANZANIA WANATAMBUA KUWA Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ndiye Kiongozi Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Nchi, Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote nchini, na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chama tawala kwa sasa, HIVYO BASI mkwamo wowote wa kisiasa, kijamii, kiuchumi pamoja na Sekta zote andamizi nchini yeye ndiye anayestahili kulalamikiwa akiwa wa kwanza.

Ninawaombeni sana na kuwaasa vijana wenzangu wa CCM kuwapuuza viongozi wote wa chama chetu wanaoendelea kutoa matamko ya kudhoofisha jitihada za mabadiliko katika sheria za uchaguzi nchini kuelekea uchaguzi Mkuu na wengine kutumia nguvu ya dola kuwadhibiti wana vuguvugu hao wenye mlengo mwema.

Wana CCM tukumbuke kuwa ni Wajibu wetu ; -

1. Kutumikia Nchi yetu na watu wake wote kwa kutekeleza wajibu wetu bila hofu, chuki wala upendeleo wa nafsi zetu, rafiki au jamaa zetu.

2. Kujitolea nafsi zetu kuondosha Umasikini, Ujinga, Maradhi na Dhuluma, na kwa jumla kushirikiana na wenzetu wote katika kujenga Nchi yetu.

3. Kuwa wakati wote wakweli, waaminifu na raia wema wa Tanzania.

Vijana wa CCM, tuungane na Wana CCM wote nchini katika kuyabiri mabadiliko ya kweli katika sheria za uchaguzi kwakuwa siyo tu kwa Watanzania lakini pia zina madhara makubwa ndani ya chama chetu na kwa kizazi kijacho.

MWISHO KABISA, TUUNGANE KWA PAMOJA KUWAKATAA ; -

1. Viongozi wa chama chetu wasiotosheka na waliotawaliwa na tamaa katika maeneo yetu na ndani ya nchi yetu.

2. Viongozi wa chama chetu wasiopenda kueneza matunda ya uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Kauli mbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION waliyo nayo wapinzani wetu (CHADEMA) haipaswi kubezwa na viongozi wachache ndani ya Chama chetu cha CCM bila ya wao kutuambia na kutuweka wazi kuwa ; -
1. Wanaibeza kwa nini ?

2. Ni Wanachama wangapi wa CCM wameridhika na kuridhia kwamba Mageuzi siyo lazima katika sheria za nchi yetu ilhali hata ndani ya chama bado fukuto la teuzi na hofu ya kukatwa majina ni kubwa na chanzo ni kukosekana kwa Reforms ?

3. Kwanini Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa (Mheshimiwa Rais) ameminya demokrasia ya Watanzania na vyama vingine vya siasa nchini kinyume na matakwa ya katiba ya CCM inayomtaka kiongozi kueneza matunda ya uhuru kwa WANANCHI WOTE ?

4. Je kuna umuhimu wowote wa kuwa na Demokrasia ya Vyama vingi katika nchi hii ?

5. Kama mbinyo huu wa Uhuru wa Kisiasa na Kidemokrasia ulipo na unaoendelea nchini kwa sasa hauna baraka za Katiba ya CCM ambayo ndiyo sheria mama ya chama chetu, Je haya yanayoendelea ni kwa manufaa ya nani au Kundi gani ndani ya CCM ?

Vijana wa CCM, Wana CCM na Watanzania tuungane kwa pamoja katika kudumisha utawala wa sheria ikiwa ni pamoja na kushinikiza Mabadiliko ya sheria za Uchaguzi katika nchi yetu.

Taifa haramu hutokana na mifumo haramu ya kisheria na kisiasa lakini Taifa halali ni lile pekee linalotokana na nguvu ya utashi wa wananchi kupitia michakato halali ya kidemokrasia na katika chaguzi zake.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI .......................!
 
Ni kikundi cha watu wachache ambao wame capture chama, na wame capture state. Why hawataki changes? Its simple ita vuruga mipango yao, na vizaz vyao for years to come

It not kwa ustawi wa nchi, ni ustawi wao
 
Hata mimi pia nina kadi ya ccm! Ila siungi mkono ubabe wa kijinga, dharau, na kejeli dhidi ya wapinzani! Siungi mkono umungu mtu ndani ya chama, na pia chama kumilikiwa na kikundi cha watu wachache na familia zao, marafiki zao na jamaa zao!
Hoja yako ina mashiko. Hivyo naiunga mkono.
 
Kikundi cha wachache kwa ubinafsi wao wamejificha ndani ya chama wanapiga hela kwa kutumia utawala ulìopo ndio wachache wasio taka mabadiliko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…