SoC02 Kama kijana ungependa upitie mlango upi kisiasa UVCCM au BAVICHA?

SoC02 Kama kijana ungependa upitie mlango upi kisiasa UVCCM au BAVICHA?

Stories of Change - 2022 Competition

Zube jr

New Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Siasa ni maisha,siasa ni kazi siasa ni imani ya kiitikadi katika nafsi ya mtu.Ili uwe wanasiasa yakupasa uwe mtu mwenye ujasiri wa hali ya juu na mwenye kujiamini kwa kila jambo lakini kwa kufuata taratibu na sheria za nchi husika.Nchi nyingi duniani zinapata utawala kupitia vyama vya siasa kiwe tawala au upinzani kulingana na sera zao wanazozinadi.

Nchini Tanzania kuna vyama vingi vya siasa kama vile CHAUMA,TADEA,ACT-WAZALENDO,CUF,NCCR-MAGEUZI,CCM,CHADEMA n.k,ambapo chama tawala ni CCM.Lakini mbali ya CCM kuwa ni chama tawala, CHADEMA ndicho chama kinachoonekana kina upinzani mkubwa kuliko vyama vingine nchini na vyama vyote katika kuwaamini vijana vikaunda umoja wao ambao ni BAVICHA na UVCCM.

1.UVCCM
Ni umoja wa vijana chama cha mapinduzi ,umoja huu naamini ulianzishwa kwa lengo la kuwapa fursa vijana kujikita katika siasa na mapenzi ya chama chao hali ya kuwa bado ni vijana lakini pia utetezi wa chama chao pale kinapokosolewa na kujifunza uongozi.

(i)Utawala
Katika hii miaka ya karibuni viongozi wa CCM waliona ni bora kuanza kuamini katika vijana juu ya kuwapa uongozi maeneo mbalimbali kama vile ukuu wa mkoa,wilaya n.k. lakini baadhi yao hawakuonekana kufanya vizuri na kotolewa.

(ii)Hoja zao
Mara nyingi binafsi naona wanajikita zaidi katika kutetea maslahi ya chama pale wanapokosolewa na si kujenga hoja juu ya viongozi wao au utawala wa chama chao.Hivyo huonekana kama hawana nguvu licha ya kuwa ni chombo muhimu katika chama.

(iii)Ushirika wao katika jamii
Ni dhahiri kuwa wanashirikiana vyema na jamii katika nyanja mbali mbali ,ushauri, msaada na kutoa mapendekezo nini kifanyike katika jamii husika.Pia wako katika ushirika wa vyuo mbali mbali nchini.

(iv)mvuto katika jamii
kwa maono yangu wanamvuto kiasi katika jamii hivyo watafute namna nzuri ya kuwashawishi wanajamii ilibwaweze kueleweka kwa ufasaha.


2.BAVICHA
Ni baraza la vijana chadema umoja huu pia naamini ulianzishwa juu ya kuwapa fursa vijana katika siasa na kuwapika ili waje kuwa viongozi bora wa baade.

(i)Utawala
Katika utawala chadema ni kama chama kikuu cha upinzani hivyo hakijawahi shika dola ila kiutawala wapo viongozi wanaokiongoza kwa mujibu wa katiba na sheria zao.

(ii)Hoja zao
Mara nyingi hujikita katika vitu mbali mbali kama vile kukosoa katiba iliyopo,tume ya uchaguzi,uonevu wa watawala dhidi yao Na kutokuwa na uhuru wa kujieleza.Hoja zao wanaamini zinamashiko lakini wakipata namna nzuri ya uwasilishaji huenda wakafanikiwa kuzifikisha kifasaha.

(iii)Ushirika wao katika jamii
Ni dhahiri pia nao ni washirika wazuri katik masuala mbali mbali ya kijamii kama vile kutoa ushauri,msaada n.k lakini pia wako na ushika na vyuo mbalimbali nchin

(iv)Mvuto katika jamii
Kwa maono yangu mvuto wao ni mdogo katika jamii hivyo watafute namna nzuri ya kuwashawishi wana jamii ili waeleweke kwa ufasaha.

Je kama kijana ungependa upitie mlango upi kisiasa UVÇCM au BAVICHA?
 
Upvote 0
Back
Top Bottom