Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Makamba katamka Kikwete ni Mtaji wa CCM, ni CCM ipi Makamba anaizungumzia?
Je ni nani mmiliki wa CCM aliyetupa Mtaji Kikwete na ni nani mvuna Faida ya Mtaji Kikwete?
Je ni Mafisadi ambao ndio wametupa Mtaji Kikwete na watavuna Faida yote?
Yetu macho, masikio na pua!
Je ni nani mmiliki wa CCM aliyetupa Mtaji Kikwete na ni nani mvuna Faida ya Mtaji Kikwete?
Je ni Mafisadi ambao ndio wametupa Mtaji Kikwete na watavuna Faida yote?
Yetu macho, masikio na pua!
Mwacheni Kikwete, ni mtaji - Makamba‏
Imeandikwa na Na Halima Mlacha; Tarehe: 4th December 2009 Habari Leo
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba amesema kamwe hawawezi kumtosa Rais Jakaya Kikwete katika Uchaguzi Mkuu ujao, kwa kuwa kiongozi huyo ndio mtaji pekee kwao.
Pia Katibu huyo amewarushia shutuma nzito wale wote walioukandia uongozi wa Rais Kikwete, ikiwa ni pamoja na kutaka asisimamishwe mwakani kuwania nafasi ya urais na kudai kuwa wana chuki binafsi na kwamba wanatumia njia hiyo ili kuwasimamisha watu wao wanaowataka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Makamba alisema Rais Kikwete ni mtaji mkubwa wa CCM uliothibitishwa na utafiti mbalimbali zilizofanywa nchini; akitoa mfano utafiti wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) wa mwaka 2008 na utafiti wa Shinovet wa Juni mwaka huu.
Alisema katika utafiti wa Redet ulionesha kuwa Rais Kikwete anakubalika na wananchi kwa asilimia 78.5 na Shivanet ilionesha anakubalika kwa asilimia 86.
Aidha, kwa upande wa vyama Redet ilionesha CCM inakubalika na wananchi kwa asilimia 72.8 wakati Shinovet ilionesha chama hicho kinakubalika kwa asilimia 69.
"Utafiti huu unaonyesha wazi kuwa CCM hatuwezi kamwe na wala hatuna mpango wa kumtosa katika kinyang'anyiro cha mwakani Rais Kikwete kwa kuwa ni maarufu kuliko hata chama chetu, huwezi kumtosa mtu kama huyu na wanaosema hivyo ni wehu wasioitakia mema CCM," alisema Makamba.
Aliwataja waliosema Rais Kikwete atoswe kuwa ni aliyekuwa Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu, Mateo Qares na Waziri mwingine katika Awamu ya pili, Mussa Nkhangaa ambao alidai wana chuki binafsi.
"Hawa wote sisi tunawafahamu…walikuwa wakuu wa mikoa wenzangu, hawana lolote ni wehu tu wanapotaka CCM tumtose Kikwete, walikuwa na mgombea wao 2005 sasa wanasema Kikwete atoswe ili wamsimamishe wakwao mwakani watajiju," alisema mwanasiasa huyo mkongwe ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa.
Alisema Nkhangaa aliwahi kuwa Mbunge wa Singida Kusini na alijaribu mara mbili kuwania nafasi hiyo bila mafanikio wakati Qares naye yalimshinda kwao.
"Jamani sasa hawa hadi kwao yanawashinda sembuse katika hili? Hata Biblia inasema mheshimu baba na mama yako ili uongeze siku zako duniani, lakini hawa wanafikia kumtukana rais," alisema.
Alisema sababu ambayo wametoa ili chama kimtose rais iwapo hatachukua uamuzi mgumu dhidi ya mafisadi si ya msingi kwa kuwa tayari Rais Kikwete ameshaanza kuwachukulia hatua wote waliotuhumiwa na ufisadi.
"Hivi rafiki yako ambaye ulikuwa naye kwenye Baraza la Mawaziri anatuhumiwa kosa na unatoa amri ashitakiwe huo si uamuzi mgumu?", alisema.
Pamoja na hayo, alikanusha hoja ya Nkhangaa aliyedai CCM kwa sasa ni chama cha matajiri na kuongeza kuwa chama hicho kina wanachama matajiri.
"Huyu anatoa hoja hii kwa kuwa ana hasira na ugomvi na matajiri hasa Mohammed Dewji ambaye alimbwaga kwenye kura za maoni, hakuna chama tajiri ila vyama vina wanachama matajiri," alifafanua.
Hivi karibuni katika kongamano la siku tatu la kujadili mustakabali wa taifa lililoandaliwa maalumu kwa ajili ya kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Nyerere, viongozi hao Qares na Nkhangaa walinukuliwa kwa nyakati tofauti wakiainisha kasoro zilizomo ndani ya chama na serikali kwa ujumla.