Kingsharon92
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 7,843
- 10,321
KweliDogo umenigusa....
Duh we jamaaTulia wewe! Kama unaona uchungu mfuate huko, mwenzio kakimbia msala.
JibuNimezipenda hoja zako si kwasababu ni nzito sana , bali ni kwasababu zina maswali magumu unayoyapatia majibu rahisi sana. Mwl Nyerere aliwahi kusema kwamba watanzania ni watu wa ajabu sana kwasababu wana majibu rahisi kwa maswali magumu sana. Nami nasema usemi huo ni wako muandika thread hii.
Kwa mfano unashangaa watu waliokuwa wakimuunga mkono sana Magu leo wamemgeuka na hata miradi yote iliyokuwa inatajwa ni kama haipo/haikufanywa. Umeenda mbali zaidi na kumtaja Ndugai kwa kushangaa kwanin bandari ya Baga-yo haikujengwa. Na na na............
Swali langu kwako ni moja tu, sijui mwenzetu ulikuwa wapi kati ya 2015-2020? Kwa sababu katika kipindi hicho sauti ilikuwa moja tu na kila aliyejaribu kufungua kinywa cha alikipata cha mtemakuni. Hivyo ulitaka Ndugai wakati ule aseme nini? Na hapo ndio utafahamu umuhimu wa kuwapa watu wako uhuru wa kuzungumza na kutoa mawazo yao amaye pengine ni tafauti nawe.
Hayati Magu, nilimpenda lakini doa kubwa lililoniudhi ni kuwabana wanataaluma kuzungumza wanayoyaju. Kilichompata Prof Assad si kikla mmoja anaujasiri namna hiyo, na wataalam wengine wengi tu waliosahau taaluma zao, kisa eti kuna simba mmoja tu anayojua kila kitu.
Swali langu ninalojiuliza mwenyewe ni moja tu; Hivi Hayati ukali wote ule juu ya wanataaluma (Kuzuia takwimu n.k), alikuwa anaogopa nini? Au alikuwa anaficha nini? Kama kulikuwa alichokificha, pengine ndicho kinachoanikwa hapa hadharani leo. Endelea na uchambuzi wako bila kusahau maswali hayo makuu na utupe jibu. Alamsik!
Ni haki yako kuchangia. Lakini kusema mzee mwana kijijiKaka huijui vizuri system ilivyokaa, na inaonekana ni aidha haujamwelewa CAG au akili yako ndogo kuchanganua mambo. Tafuta mtu mwenye uelewa mzuri akuelekeze hali halisi ilivyo
Umetoa madai meeeengi! Lakini ushahidi sifuri!Hivi unatumia nini hasa kufikiri?
1) wote waliompinga Magu walishughulikiwa. Tundu Lissu aliyemchambua kama karanga. Risasi 38, na amesurvive kwa muujiza wa Mungu tu. Ben Saanane aliyetilia mashaka PhD ya Magu, na kwa kweli wanataaluma wengi tu walioshuhudia muda aliotumia maabara pale idara ya kemia UDSM, waliosoma nae kabla, wana mashaka na hiyo PhD, Ben Saanane alipotezwa, tena alishapewa warning kabisa.
2) waliokuwa na hoja tofauti na zake, walikiona cha mtemakuni. Wabunge waliopinga mkakati wa Magu kuzipiga hela za Cashewnut Fundzote, baada ya kuzinguana aliponyofoa B. 200 za mfuko huo, wakamtaka azirudishe, yeye akaleta muswada wa kuzipiga zote. Walipolalamika akatishia kuwatimua wote, pamoja na waziri mkuu. Na pia akatishia 'kuanza na shangazi zao'.
3) waliodiriki kuongea kitu tofauti na msimamo wake, walitumbuliwa. Kuna yule msajili wa hazina, somebody Mafuru, aliyejaribu kufafanua ugumu wa kufisidi fedha zilizowekwa Deposit, alitumbuliwa. Dr. Likwelile aliyeshauri mradi wa kuhamia Dodoma usubiri next budget , baada ya Magu kuutangaza mara baada ya kuukwaa uenyekiti wa ccm, bajeti ishapitishwa.
4) alikuwa tayari kufanya kazi na waliosifu na kuabudu tu. Mwanzoni Ndugai alijikuta yuko chini ya Naibu Spika ambaye alipokea maelekezovmoja kwa moja toka ikulu. Ndugai akaamua kuunga mkono juhudi. Akaingizwa kwenye good books za Magu.
Huyo Samia mwenyewe mara kadhaa tulisikia nusura aachie ngazi. Naona alitafuta namna ya kuishi na ugonjwa huo unaoitwa MaguSyndrome. Wengi wa hawa, walioishi na ugonjwa huo, mara baada ya kifo chake, wamerudisha akili zao.
Binafsi siwalaumu. Katika mazingira hatarishi, mtu ana haki ya kujilinda. Katika tawala za kistaarabu, mkitofautiana unajiuzulu. Kwa Magu ni visasi.
Magu hajachafuliwa, amejichafua mwenyewe, hawa wengine walikuwa mateka wa Magu. Na ni wengi sana
Nimemsifia nani?! Tunachosema JIWE NI MWIZI, PERIOD! Hana tofauti na hao wengine! Na miradi mingine ambayo anasifiwa na misukule wake, kaikuta! Mradi mpekee "aliouasisi" yeye kama yeye ni ununuzi wa ndege!! Lakini cha ajabu hata hizo ndege alizinunua bila kuwapo comprehensive business plan! Na kuna kila dalili kwenye ndege nako kumejaa wizi ndo maana Wakala wa Ndege akaihamishia Ikulu, and since then haikuwahi kukaguliwa! Sasa kama ni msafi alikuwa anaogopa nini kuweka mambo wazi?!Acha kutoa povu.
Kwa hiyo ameondoka na kuiacha nchi kama ilivyokuwa 2015?
Hao wengine unaowasifia waliyafanya kwa pesa kutoka mifukoni mwao?
Sasa maamuzi hayo yangemsaidia nini mtanzania? Si wakati wowote utatuzi wa matatizo hutatuliwa kwa maamuzi mamoja? Jifunze kitu katika hili, usipitwe na wakati.Jibu
1. Mtei- alimbishia Nyerere na kujiuzulu
2. Balali - alijiuzulu akarudi zake marekani
3. Assad - aliondolewa baada ya kusema ukweli
Ndugai hata Mama Samia kama walikuwa hawakubaliani wangetoa mawazo yao. Wabaki au wafukuzwe au wajiuzulu huo ndiyo uungwana
Hayo mambo ya korosho yoote yalizungumzwa Bungeni, tena kwa detail nyingi tu akina Hawa Ghasia, Nape Nnauye, na Bwege. Magufuli alitoa vitisho hadharani, kauli zoote nilizonukuu.Umetoa madai meeeengi! Lakini ushahidi sifuri!
Nothing new. Not impressed.
Unasema kuhamia Dodoma ilikuwa ni kukurupuka. Hivi unajua plan ya kuhamia Dodoma ilikuwa ni ya mwaka gani?Kwanza kuhamia dodoma ilikuwa kukurupuka kwa jpm. Ndo Mana hela zote zikaelekezw huko huku ajira zikitoweka maazima. Sema ni hivi jpm alikuwa mtu hatari Sana na alikuwa Yuko radhi watu wote wafe ila yeye apatr ujiko tu. Watu wanasuffer mtaani kwa kukosa ajira miaka yote sita. Hata madaktari ambao tulizoea kipindi Cha jk wanaajiliwa bila kubaki lakini nao wanaendesha bodaboda na anajisifu eti ni rais wa wawanyonge. Mungu asingemchukua au akina jk wasingefanya yao nchi nzima ingejaa wamachinga.
Binafsi huyu CAG simuamini kamwe.
Akiwa CAG BANDARI YA BAGAMOYO HAKUONGEA, PRES YAKE YA JANA HAJARUDIA KUZUGUMUZIA BUNGE NI DHAIFU AU ANASUBIRIA SPIKA ASTAAFU? [emoji23]Umetoa madai meeeengi! Lakini ushahidi sifuri!
Nothing new. Not impressed.
Alimbishia JK kuhusu kubomoa jengo la TANESCO. Ikabidi aamrishwe kusitisha ubomoaji.Sasa maamuzi hayo yangemsaidia nini mtanzania? Si wakati wowote utatuzi wa matatizo hutatuliwa kwa maamuzi mamoja? Jifunze kitu katika hili, usipitwe na wakati.
Kwani Magu Miaka 20 aliyokuwa waziri alimbishie mkuu ganu wa nchi?
Ili muwashukie kwa masifa yenu na muanze kuwapa majina ya vibaraka ohh sijui wanatumiwa na mabeberu? Wapinzani toka mwanzo walisema serikali ya awamu ya tano haina uhalali wa kuongoza wananchi, ninyi wafia madaraka mliwajibuje vile...?Iwavyo vyovyote kama alisimama pale hadi jamaa anatutoka maana yake alishirikiana nae. So na yeye ni mwizi tu. Kama wanadhani kumchafua JPM kutawaacha wao salama basi wanajidanganya. Kichekesho ni kuwa hata wapinzani nao wameungana kutuchezea hii futuhi,wangesimama pembeni na ngojera hizi then wakaenda kwa wananchi kuwaambia tu kuwa kama rais alikuwa hivi basi na mfumo mzima wa ccm ukijumuisha hawa waliobaki wote umeoza tuutoe kuweka wengine wangepata sapoti kubwa sana. Sasa kwa sababu wanaongozwa na chuki binafsi kwa mwendazake hata fursa hii waneshindwa kuitambua wamejiunga
Vyovyote iwavyo kama alisimama na jamaa hadi mwisho anahesabika kuwa alikubaliana na kilichotokea
Acha mihemuko,unafikiri kwa nini Mungu alitusaidia afe mapema???Ukisoma mitandao ya kijamii hasa twitter utafikiri kweli hii nchi imeibiwa kila kitu na hakuna kitu kimeachwa, kumbe sio kweli.
Watu wanajifanya kushangaa ATCL kupata hasara, hivi mtu mwenye akili timamu unaweza kushangaa atcl kupata hasara? By the way, ni shirika gani la serikali linalopata faida? Lipi? Mashirika yote ni hasara kila mwaka kuanzia Tanesco, TPDC, TTCL, ATCL, NHC na mengine yote, kwa nini shida iwe kwa ATCL?
Halafu watu wanataka kusema Magufuli ange eliminate rushwa ama wizi wa mali za umma 100%, hilo jambo halipo Duniani. Duniani kote, kuanzia China ambapo kosa la rushwa unaweza kuuwawa ama Marekani ambapo mifumo iko strong bado watu wanaiba na kula rushwa, tusimsingizie Magufuli kwa kila kitu.
Kuna kikundi ama kingenge cha wahuni sijui kinalipwa na nani kutaka kumchafua Magufuli na report ya cag
Pole, kwasababu huhitaji tafsiri nyingine au ushuhuda kuwa bunge limedhihirisha sasa hivi kuwa lilikuwa dhaifu baada ya Spika wake kutoa matamko kama ya Bandari ya Bagamoyo yakipingana na matamko yake wakati ule. Muhimili wake ndio uliokuwa na uwezo wa kuiuliza serikali kimaandishi ili apate ufafanuzi kwanini mradi mzuri kama ule unapigwa chini.Akiwa CAG BANDARI YA BAGAMOYO HAKUONGEA, PRES YAKE YA JANA HAJARUDIA KUZUGUMUZIA BUNGE NI DHAIFU AU ANASUBIRIA SPIKA ASTAAFU? [emoji23]