Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kwanza niipongeze serikali Kwa kufuta huo mswada wa kutaka kuwabeba polisi ati wasishtakiwe wakiwa kwenye majukumu Yao.
Ingekuwa muswada wa hovyo kuwahi kutokea.
Sisi waalimu nasi tungepeleka muswada bungeni kuwa tusishtakiwe tuwapo kwenye majukumu yetu, tukiwapa adhabu wanafunzi, Kama mnavyojua waalimu Kama Mimi tunapiga bakora mpaka mtoto anazimia Kama sio kufa Kabisa. Ni vile sheria zinatuzuia kufanya hivyo.
Hasira za mishahara kidunchu tungezihamishia Kwa watoto, hasira za kutopandishiwa mishahara na madaraja tungezihamishia kwenye michongo na matako ya wanafunzi. Ni bahati tuu sheria zinatukataza.
sisi madaktari nasi tungepeleka muswada kuwa tusishtakiwe iwapo itatokea uzembe WA bahati mbaya au Makusudi tunapowahudumia wagonjwa. Mbona watoto wenye utindio wa ubongo wangeongezeka nakuambia, hakuna cha uzembe wala nini, tungefanya kusudi kabisa.
sisi tume ya uchaguzi tungeiomba serikali ituwekee sheria zitakazotulinda katika majukumu yetu, hatutaki kushtakiwa, hata Kama tukimpa ushindi asiyemshindi,
Kada zingine nazo zingedai sheria zakuwalinda wawapo katika majukumu Yao hata kama wamefanya uhalifu wa makusudi kabisa.
Na mwisho tungekuwa na taifa la kulindana.
Natamani hata kina Spika, Rais na wengineo ambao wanakinga ziondolewe ili wote tuwe Sawa chini ya sheria.
Tupendane!