WilsonMwalukasa
Member
- Dec 26, 2021
- 33
- 23
Kiswahili na Kiingereza, ni lugha mbili ambazo zipo kwenye mitaala ya elimu yetu nchini, lakini asilimia zaidi ya 80 ya watanzania hawajui lugha zote mbili Kwa ufasaha.
Au hata lugha Moja tu kwa ufasaha na usahihi.
Ni kwa sababu ya uwepo wa lugha mbili ambazo, hupokezana na huingiliana kwenye mitaala ya elimu.
Shule ya msingi utatumia Kiswahili, Secondary na chuo utatumia Kiingereza.
Kama tumeweza kutumia lugha ya kiswahili, kwenye elimu ya shule ya msingi tumeshindwa nini ngazi ya sekondari na chuo?
Mtanzania akiwa na wazo, hawezi kulipeleka katika lugha ya kiswahili na kiingereza pia, ni kwa sababu hazijui lugha zote Kwa ufasaha.
Mkanganyiko huu wa Lugha ni moja wa kikwazo, Cha maendeleo ya uchumi wa taifa letu.
Lugha yetu ya taifa, ni kiswahili. Lakini Kiswahili hakifanywi vile ambavyo inabidi ifanywe lugha ya taifa iwe.
Serikali imeshindwa kuzuia swala Hilo na kama sio kuzuia, basi imeshindwa kuzipatia kipaumbele lugha zote mbili kwa wakati mmoja.
Kama serikali imeifanya kiswahili kuwa lugha ya taifa, basi inabidi ihakikishe yafuatayo.
1. Kiswahili kitumike ngazi zote za Elimu za elimu nchini Chekechea Hadi ngazi ya chuo kikuu, na kusiwe na Muingiliano wa lugha ya kiingereza.
2. Serikali ihakikishe matumizi ya lugha ya kiswahili kwa ufasaha, lugha ya kiswahili itumike kwa upana katika kutekeleza majukumu yake.
Leo unakuta tangazo la au nyaraka ya serikali Kwa kiingereza. Serikali imeshindwa kuwa mfano Kwa wananchi wake katika matumizi ya lugha ya kiswahili.
3.Bila ubabaishaji serikali ikazanie lugha ya kiswahili, iwe lazima kujifunza Kwa Kila mgheni ajae nchini.
4.Mitandao ya kijamii, vyombo vya habari na vifaa vya mawasiliano, vyote Kwa ulazima wa kisheria vitumie lugha ya kiswahili TU.
Pili kama serikali imeamua lugha zote mbili zitumike, basi inabidi ihakikishe haya.
1: Lugha zote mbili zipewe kipaumbele kuanzia ngazi ya utoaji elimu, jamii na hadi serikalini.
Na kiujumla serikali imeshindwa kupanua na kutengeneza fursa za ajira kupitia Kiswahili.
Kupitia balozi zetu zilizopo mataifa mbali mbali duniani, serikali ingeweza kuandaa programu za kufundisha kiswahili, walimu wangeajiriwa watanzania.
Viongozi katika serikali zetu, wanashindwa kuwa innovative na creative, wamakalia kutuahidi haki zetu au majukumu ya serikali.
Ahadi za kampeni ni nitajenga Barbara, nitajenga shule kiundani hayo ni majukumu ambayo serikali imeshindwa kutekeleza.
Ni ngumu kusikia ahadi za ubunifu, ambazo zitamkwamua mtanzania.
Viongozi wangeweza kubuni programu ya kukuza lugha ya kiswahili na kuifundisha, wapo watu wengi wanataka kujifunza kiswahili hawajui wapi pa kuanzia.
Kama tumeamua tuwe taifa la lugha malaya, yani tuwe na lugha mbili basi zote zipewe kipaumbele.
Mtanzania ashindwe akatae yeye kujifunza lugha zote mbili, Kwa Sasa serikali ndio imeshindwa kumjengea mazingira ya kujifunza lugha zote mbili.