Kama kodi ya jengo inalipwa kupitia LUKU, wanaotumia umeme wa jua (solar) hawatalipa kodi ya majengo?

Kama kodi ya jengo inalipwa kupitia LUKU, wanaotumia umeme wa jua (solar) hawatalipa kodi ya majengo?

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Ukiacha tatizo la nyumba moja kuwa na zaidi ya LUKU moja na mpangaji kumlipia kodi ya jengo mwenye nyumba, kuna hili la majengo yasiyo tumia umeme wa Tanesco watalipaje kodi ya majengo yao au wao wana utaratibu wao wa kulipa Property Tax.
 
Wamesema wasio na umeme watalipa kwa utaratibu wa zamani (wa kupanga foleni bank i think)
 
Ukiacha tatizo la nyumba moja kuwa na zaidi ya LUKU moja na mpangaji kumlipia kodi ya jengo mwenye nyumba, kuna hili la majengo yasiyo tumia umeme wa Tanesco watalipaje kodi ya majengo yao au wao wana utaratibu wao wa kulipa Property Tax.
Mtalipa, sola ni nishati ambayo iko chini ya Wizara ya Nishati na pia Mazingira hivyo hauwezi ukakaa tu unafyonza nishati bure.
 
Kuna namna watumia solar nao watabanwa ktk Tozo.

Twiga amechachamaa, Anahitaji kukamilisha alichokikusudia.

Anakaba popote kama mkata umeme.
 
Pesa inayopatikana kupitia LUKU haina haja ya hao kulipa.
Kuna fremu za biashara kila mtu anatumia meter yake.
Chukulia ni fremu 5 zipo kwenye kiwanja kimoja.
Hapo ni shiling ngapi? Hata wasipolipa ni sawa.
Hii nchi ni tajiri sana.
 
Kiuhalisia kabisa hatulipii kodi ya jengo bali tunalipia tozo ya luku,
Katika jengo moja lenye frem 10 na kila frem inajitegemea luku yake kila mita ya luku itakua inalipia kodi yake, hapo itakusanywa kodi ya majengo 10 wakati yapo katika jengo moja.
 
Pesa inayopatikana kupitia LUKU haina haja ya hao kulipa.
Kuna fremu za biashara kila mtu anatumia meter yake.
Chukulia ni fremu 5 zipo kwenye kiwanja kimoja.
Hapo ni shiling ngapi? Hata wasipolipa ni sawa.
Hii nchi ni tajiri sana.
Kodi hii haitozwi kulingana na idadi ya mita bali, jengo hata kama jengo lina mita 10, itakayolipia kodi ya jengo hilo ni mita moja tu, mwenye nyumba anatakiwa kutoa taarifa ni mita ipi ndio itakuwa inakatwa tozo hiyo.
 
Back
Top Bottom