Kama kuna aliyewahi kufanya manunuzi ali express naomba experience

Kama kuna aliyewahi kufanya manunuzi ali express naomba experience

Jamani kama kuna aliyewahi kufanya manunuzi ali express naomba experience jinsi wanavyo fanya kaz
Angalia bidhaa, soma maelezo kwa makini sana kisha uki afford nunua kwa kutumia mpesa visa card, Airtel Mastercard au bank inayoruhusu online malipo.

Kwenye kununua bei ya bidhaa utaangalia total kwenye cart kisha unaweka pesa kwenye hizo kadi ongeza kiwango kufidia makato

Mfano bidhaa ni 10000 weka 14000
Au 13k otherwise kama unajua makato ya bank, mpesa au Airtel.

Ukiona iphone 15 pro inauzwa kwa elfu 50 soma vizuri sio iphone hiyo inaweza kuwa ni accessories

Narudia soma maelezo na bei na jikite kwenye uhalisia sijui unanunua kwa matumizi au kuuza ? Kama ni kuuza tumia Alibaba
 
Nimewahi kununua vitu na ninaendelea kununua, nimejifunza yafuatayo
  1. Angalia sana spelling na bei katika bidhaa unazotaka kununua mfano Kuna Xiaomi na Xioam wahuni wanakuingiza chaka unanunua kitu feki. Hapa utakuta bidhaa ambayo bei yake 700k utashangaa inauzwa 200k kuwa makini sana. Utagundua Kuna kitu hakipo sawa
  2. Soma vizuri item description, specifications na customer reviews ni muhimu. Mimi binafsi sinunui bidhaa ambazo hazina customer reviews au zikiwa chache sana au nikikuta malalamiko hata ya mtu mmoja.
  3. Bidhaa husika kuwa na idadi kubwa ya kiasi kilichouzwa zilizouzwa, hapa pia unaweza kuona maoni ya wanunuzi juu ya bidhaa hiyo.
 
Jamani kama kuna aliyewahi kufanya manunuzi ali express naomba experience jinsi wanavyo fanya kaz
Fanya hivi:
  1. Fungua akaunti huko AliExpress.
  2. Weka anuani yako ya kupokelea bidhaa zako.
  3. Chagua namna ya kulipia bidhaa zako. Mfano unaweza tumia prepaid card (NMB bank watakufungulia hii), Master card ya M-pesa au Airtel money, nk.
  4. Ukitaka kununua bidhaa yoyote ile zingatia vitu vifuatavyo kabla hujalipia bidhaa hiyo:
    • Description ya bidhaa
    • Review za Wateja (ni Muhimu sana hapa), maana Wateja Huwa wanaeleza ukweli kuhusu bidhaa husika.
    • Specifications za bidhaa husika.
    • Rate ya muuzaji. Je, anapewa star ⭐ ngapi katika bidha zake?
    • Mengine watakueleza wananzengo
  5. Ukilizika na bidhaa na maoni ya wanunuzi wengine, ndipo bonyeza sehemu iliyoandikwa "Buy". Hapo itakupeleka Moja Kwa Moja sehemu ya kulipia.
  6. Hakikisha Kuna kiwango Cha kutosha Cha Pesa katika akaunti yako. Kwa mfano, radio 📻 inauzwa Tshs 100,000/= kwenye akaunti yako iwe Kubwa Kuliko Tshs 100,000/=.
  7. Ukishalipia Subiri mzigo wako kupitia Kwa wakala. Mfano speedaf, posta, DHL, n.k
Note: usipokuwa makini unaweza kuuziwa kitu tofauti na matarajio yako au na jinsi ulivyokiona katika picha..
 
Nimewahi kununua vitu na ninaendelea kununua, nimejifunza yafuatayo
  1. Angalia sana spelling na bei katika bidhaa unazotaka kununua mfano Kuna Xiaomi na Xioam wahuni wanakuingiza chaka unanunua kitu feki. Hapa utakuta bidhaa ambayo bei yake 700k utashangaa inauzwa 200k kuwa makini sana. Utagundua Kuna kitu hakipo sawa
  2. Soma vizuri item description, specifications na customer reviews ni muhimu. Mimi binafsi sinunui bidhaa ambazo hazina customer reviews au zikiwa chache sana au nikikuta malalamiko hata ya mtu mmoja.
  3. Bidhaa husika kuwa na idadi kubwa ya kiasi kilichouzwa zilizouzwa, hapa pia unaweza kuona maoni ya wanunuzi juu ya bidhaa hiyo.
Juzi nimepigwa.
Niliagiza Huawei WiFi router, specifications zote ni 4G.
Niliyoletewa ni 3G.
 
Juzi nimepigwa.
Niliagiza Huawei WiFi router, specifications zote ni 4G.
Niliyoletewa ni 3G.
Pole sana mimi nilinunua memory card ya aftatu GB 64 kuiweka kwenye simu haiwezi kuhifadhi hata faili la GB1.
Pia nilinunua Redmi note 12 safi bei kitonga baada ya kuitumia nikagundua Ina kasoro katika GPS Kuna wakati haifanyi kazi kabisa. Lakini mambo mengine Iko vizuri
 
Mi huwa nanunua mara kwa mara vitu vya bei chee lakini naweza kutumia siku2 ku select item sababu ntasoma reviews zote ya bidhaa na kuhakikisha seller ni wa uhakika kabla ya kununua , icho ndio muhimu sana , mengine ni yale yale tu

Kinachozingua hawa aliexpress wana jamaa wao wa delivery ni miyeyusho hakuna tena anakoromea sana wateja na hajali hata kidogo nishazinguana nae mara kadhaa akagoma kuniletea mizigo yangu,

Tofauti na hapo kuna muda wa kusubiri order kufika , mengine fresh na bahati inahusika pia always kuna possibilty ukapigwa na kupata refund ni 50/50
 
aliexpress cha muhimu ni kusoma kwa makini description ya bidhaa unayotaka kununua,ndivyo unavyotaka iwe? apa ndio wengi tunafeli, kingine angalia comments na rate walizotoa wateja waliowah kununua iyo bidhaa, tumia muda mwingi kusoma hivyo vitu kabla hujafanya manunuzi, nina miaka mitatu natumia aliexpress sijawah letewa kitu tofaut na ilivyotarajiwa, kingine kama wadau walivyosema ni bidhaa isome kwa makin unaweza kutana na simu imeandikwa 14 pro na inamuonekano wa iphone 14 pro tena kwa bei che ukakurupuka kuagiza kumbe ni simu ya kichina,manunuzi ya online ni kua makin,ukiwa makin utaenjoy sana yan kila kitu utataka uagize
 
Back
Top Bottom