Kama kuna Mawaziri wana 'Wataalam' hasa wa 'Vilingeni' wanaowasaidia vyema Uongozini kwa Tanzania nzima ni Kassim, Ummy na Mwigulu

Kama kuna Mawaziri wana 'Wataalam' hasa wa 'Vilingeni' wanaowasaidia vyema Uongozini kwa Tanzania nzima ni Kassim, Ummy na Mwigulu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Na nashauri hata Siku zingine ikitokea Mvua zikagoma Kunyesha tuwaombeni hawa Waandamizi Watatu tajwa katika 'Headline' yangu watusaidie Kuongea na hao 'Wataalam' wao kwani kwa muda mfupi tu huu wameshaonyesha kuwa hakika 'Ndumba' wanazijua na wanaweza.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba hakuna Watu ambao 'Madame Levy' hapendi kuendelea nao ( kutokana na sababu kadha wa kadha ) kama Majaliwa, Mwalimu na Nchemba ila kila akipanga Safu yake huwa hawagusi na nahisi huenda pia huwa anawasahau na kuja Kukumbuka kuwa hawahitaji pale Jaffary Haniu akishamaliza kutuwekea Teuzi mpya Mitandaoni.

Nashauri huko mbeleni Timu yetu ya Mpira wa Miguu ya Taifa Stars ikiwa inataka Kufuzu Kombe la Dunia tusipoteze sana muda Kuandaa Kamati mbalimbali za Ushindi bali tuwaombe tu Wataalam ( Waganga wa Kienyeji ) wa hawa Waandamizi Watatu tajwa wamalize Shughuli yote tu Kiuchawi ( Kiulozi )

Kassim, Ummy na Mwigulu Shikamooni!
 
Watu wengine bana. Fanya kazi utaonekana tu.

Nakumbuka kuna wakati niliotesha kibanda changu chap chap baadhi ya ndugu wakasema nishajiunga kwenye ushetani kumbe malengo tu na nidhamu ya hela....watu wanavimba na magari wengine tumekomaa na bodaboda na mengine mengi.

Mchawi Nidhamu Tu. Acheni imani za kijinga na kuchafua watu na Mkumbuke Mungu yupo pia.

Ukiona hupati majibu unayotaka ujue lazima kuna mahala unakosea. AMINI
 
Back
Top Bottom