Kama kuna mikopo ya masharti nafuu kwanini nchi ichukue yenye masharti magumu?

Kama kuna mikopo ya masharti nafuu kwanini nchi ichukue yenye masharti magumu?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Naomba wenye uelewa wa mambo ya uchumi wa nchi wanipanue ufahamu kidogo kuhusu mambo ya mikopo.

Nimekua nikisikia kwamba serikali imekopa au itakopa mikopo yenye masharti nafuu, na mara nyingi hatuambiwi inapokua imekopa yenye masharti magumu.

Ndipo nikahitaji ufafanuzi toka kwa wataalam wetu:

1) Mikopo yenye masharti nafuu inakuwaje?
2) Mikopo ya masharti magumu inakuwaje?
3) Kama kuna mikopo ya masharti nafuu kwa nini nchi ichukue mikopo yenye masharti magumu?
 
Mikopo yenye masharti nafuu ipo lakini huwa inaambatana na masharti yake kama:
  • Haki za binadamu
  • Demokrasia
  • Uwazi na uhuru wa vyombo vya habari
  • Utawala bora
  • Kupambana na rushwa n.k
Sasa hayo masharti Magufuli alikuwa hayawezi ndio maana ikamshinda, akawa anachukua mikopo yenye riba kubwa (commercial )
 
Mikopo yenye masharti nafuu ipo lakini huwa inaambatana na masharti yake kama:
  • Haki za binadamu
  • Demokrasia...
Sasa Magufuli kaingiaje? unajua kwa mtu ambaye haishi Tanzania anaweza kufikiri hii nchi ilikuwa na maendeleo makubwa na ni ya mfano kwa demokrasia ila Magufuli tu ndio kaja kuharibu.
 
Sasa Magufuli kaingiaje? unajua kwa mtu ambaye haishi Tanzania anaweza kufikiri hii nchi ilikuwa na maendeleo makubwa na ni ya mfano kwa demokrasia ila Magufuli tu ndio kaja kuharibu.
Hueleweki
 
Sasa Magufuli kaingiaje? unajua kwa mtu ambaye haishi Tanzania anaweza kufikiri hii nchi ilikuwa na maendeleo makubwa na ni ya mfano kwa demokrasia ila Magufuli tu ndio kaja kuharibu.
Alikuwa anajaribu kuonyesha kuwa hayo yanayoitwa masharti nafuu, ni nafuu kwa kuwa hayana ongezeko la kifedha moja kwa moja, lakini ni magumu katika utawala wa aina fulani.

Kwa mfano katika utawala wa JPM asingeweza kukubaliana na hayo ya sijui haki za binadamu, haki za waliobeba mimba kurudi shuleni, ushoga nk. na akaona ni bora kuchukua mikopo ya kibiashara ambayo sharti lake ni kulipa riba tu(manageable)
 
Alikuwa anajaribu kuonyesha kuwa hayo yanayoitwa masharti nafuu, ni nafuu kwa kuwa hayana ongezeko la kifedha moja kwa moja, lakini ni magumu katika utawala wa aina fulani....
Kilichoulizwa kwenye mada hakijajibiwa ila unaelezwa utawala Magufuli, sikuona au hakukuwa na haja ya kumtaja Magufuli maana sidhani kama haiwezekani kujibu kilichoulizwa pasina kuzungumzia utawala wa Mwendazake.
 
Back
Top Bottom