Kama kuna mtu anakosa raha kwa sababu ya Yanga mimi wa kwanza!

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mimi siyo Mtanzania ni Mkongo, ila nilijikuta nimependa timu hii ya Tanzania kuliko kawaida na aliyenivutia kwenye timu hii ni Makambo. Mwaka 2018 nilitokea kuwa na mapenzi ya dhati na uchezaji wake, nilikuwa naona clip zake nyingi YouTube.

Mpaka nikajikuta ata Yanga pia nimetokea kuipenda sana na kuvutiwa na Yanga mpaka sasa hivi. Kibaya ni kwamba kila wakati timu hii inapofanya vibaya najikutaga nina hasira ya ajabu.

Maana katika watu ambao ni waoga kushindwa mara pili au mara tatu mimi ni wa kwanza. Huwa sipendi kushindwa au kuona kitu changu chochote au ndugu, rafiki ameshindwa jambo moja mara 2 au zaidi.

Ila nilichogundua, hii timu siyo kwamba uwezo wa kufika mbali hawana, wanao ila hawana bahati tu!
 
Toa kabisa taarifa zako kamili, majina na mahali ulipo.

ili mkifungwa tukuwahi kabla hujajiua.
 
Yaani wewe ni Mcongo, halafu uumizwe na matokeo ya sare ya 1-1 ya Yanga! Nilidhani eti umeumia baada ya timu ya nchi yako, TP Mazembe kutolewa na Vipers ya Uganda!
 
WAGALATIA 5:22-23.

[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

[emoji117] "KIASI" huwezi kuteseka kwa jambo lolote lile ktk maisha.

Msidhani Maandiko Matakatifu ni hadithi za JUMA na ULEDI bali ni tiba hata kwa afya za akili [emoji1]
 

Jezi ya Yanga ni 'NZITO'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…