G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Kwa haya machache tunayoyaona, Rais wetu anavunja taratibu na kanuni waziwazi, vipi kwa tusiyoruhusiwa kuona? Tutazame haya machache:
1. Nafasi 10 alizopewa kuteua wabunge alivunja katiba tukapiga kelele mmoja akajiuzulu kisha kupewa ubalozi. Hata hivyo kujiuzulu kwa huyo mmoja hakukumoondolea hadhi ya kulipwa mafao kama mbunge.
2. Uteuzi wa Jaji mkuu alienda kinyume cha taratibu za kimahakama, akateua kaimu Jaji mkuu. Sijuia alikuwa anataka atimiziwe kwanza matakwa yapi ndipo amthibitishe? Nadhani alifanikiwa. Sasa tunaona hukumu zikiamuliwa na DPP lakini kwa kivuli cha Rais.
3. Kwenye uteuzi wa CAG mpya amevunja tena katiba waziwazi na hata hivyo ameshindwa kabisa kutafsiri neno "Shall" kisheria ambalo limo kama muongozo wa utendaji wa CAG katika kanuni zinazoongoza ofisi hiyo. Hata hivyo tunamkumbusha Rais aelewe kuwa kanuni zinazoongoza ofisi yoyote ile ya umma zimetokana na muongozo mama sheria iliyopitishwa na bunge kwa kuzingatia katiba. Kanuni hazijawahi kuwa juu ya katiba hata siku moja.
4. Kwenye manunuzi makubwa na utekelezaji wa miradi mbali mbali mikubwa ame by-pass muongozo wa bunge na ndiyo maana havikaguliwi. Huu ni ufisadi wa aina yake.
Tunamkumbusha Rais kuwa aliapa kuilinda katiba. Hakuzungumza tu pale uwanja wa Uhuru, aliapa!