Kama kweli elimu ni ufunguo wa maisha ni kwanini vijana wengi wanashindwa kutumia elimu kujiajiri kama wanavyo shurutishwa kujiajiri?

Kama kweli elimu ni ufunguo wa maisha ni kwanini vijana wengi wanashindwa kutumia elimu kujiajiri kama wanavyo shurutishwa kujiajiri?

Loading failed

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2023
Posts
2,603
Reaction score
7,501
Kumekua na sintofahamu huko duniani inayoonekana vijana wengi wasomi wakisota mitaani kwa ugumu wa maisha kuliko vijana ambao hawajaenda shule au ambao siyo wasomi wa kiwango cha juu .

Wapo vijana waliowacheka wenzao kwa kufeli shule huku wao wakifurahia kufaulu na kuendelea na masomo na baada ya miaka kadhaa ya kuhitimu wanakuja tena kushinda mitaani huku wakiwaonea wivu vijana wasio wasomi waliotusua maisha

Pia kumekua na wazee waliozeeka huko maofisini mpaka wakishika kalamu vidole vinatetemeka waki ng'ang'ania kubaki kwenye ajira badala ya kuachia ngazi vijana nao waajiriwe bali wazee hao wamekua wakiwasema vijana kutokujiajiri na kujishughulisha huku wakiwang'ong'a na kuwashurutisha wajiajiri je, wao wanashindwa nini kujiajiri.

Je , kwanini kama elimu ni ufunguo na mwanga wa maisha ni kwanini vijana wanashindwa kutumia elimu kujiajiri?
 
Shida kubwa imekuwa kwenye mtazamo wa elimu. Lengo la elimu ni kukuza maarifa, ujuzi na maadili kwa lengo la kujenga mtazamo ulio chanya katika maisha ya mwanadamu. Kwa muda mrefu elimu imekuwa imeegemea sana kwenye kujenga maarifa na kuangalia ufaulu wa masomo ya darasani na kuacha elimu ya vitendo pembeni na maadili pia. Ili elimu iwe na maana, elimu ya darasani na nje ya darasa lazima viende kwa pamoja katika umri mdogo. Watu wasome masomo yanayosukumwa na upeo na uwezo wao.
 
Unasoma ili utatue changamoto zilizopo katika jamii,lkn tatizo wengi wanakimbia changamoto,ili ni tatizo afrika hasa
 
' Elimu imekuwa kifungo cha maisha '- Jumanne Kishimba.
 
Back
Top Bottom