Kama kweli Manji unaipenda yanga achana na uenyekiti ili ujengwe mfumo mzuri wa uchumi wa klabu

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
3,183
Reaction score
3,660
Watanzania akili zetu zimelala sana wanao taka Manji aendelee kuwa mwenyekiti sio kama ni Kiongozi mzuri ila eti ni kwa sababu ana pesa

Hayo mambo yamepitwa na wakati kilabu kubwa kama Yanga kuka tu kumtegemea mtu awe anatoa tu pesa bure bure wakati zipo njia nyingi za kufanya na kilabu ikaweza kujitegemea

Ina sikitisha kuona mijitu ambayo wenyewe ndio wanajiita wadau wa mpila wakiwa wanafikilia kuendesha kilabu kubwa kama Yanga kwa kutembeza bakuli

Huo mfumo wa kuendesha kilabu kwa kutembeza bakuli umesha tumika kwa miaka yote na hadi Leo kilabu haina mafanikio yoyote ila bado kuna watu mibichwa yao imeganda na jasho linawatoka kutoka Manji arudi eti kwa sababu anapesa hivyo atakuwa anatoa tu pesa bure bure kama mtu anampa mkewe

Manji usigombe uenyekiti na wala usitoe hata shilingi kumi ya kusajili mchezaji wala kulipa mishahara ya wachezaji maana hapo utakuwa huisaidii Yanga bali unazidi kuipoteza na kufanya mashabiki na viongozi mibichwa yao aendelee kulala

Kama kuna mtu hadi Leo hajui umuhimu wa kilabu kubwa kama Yanga kuwa kampuni basi ni bora uachane na kushabikia mpira maana hauna tofauti na mtoto aliyezaliwa jana
 
Timu haina uongozi unaoeleweka haitaki kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti kivuli.
Jamaa kasema hataki watu wamebakia ohh wewe ndio tunakutambua.
Hakuna mtu atatoa pesa za bure. Alipotaka kuanzisha kampuni mlimwambia awaachie Yanga Yenu.
Leo imebakia bakuli na shukuruni TFF na bodi ya ligi kuwalindeni kwa ratiba mkaanza nyumbani.
Mkianza kwenda mikoani kwa bakuli mtaipata.
 
hii habari kandambili hawataki kuisikia
 
Mimi mwenyewe mwanayanga kindaki ndaki.. ila Manji simkubali... niliwai andika barua humu kuhusu mabadiliko ya Yanga

habari wanayanga wote.

huu ujumbe nitashukuru sana tukiutoa kwa pamoja kwa kuweka maoni yetu kwa timu yetu pendwa..

najua wengi tunaona yanayotokea kwa timu yetu.. mishahara ya wachezaji, gharama za usafiri na mengi yamekuwa kitendawili kisa tajiri wetu mpendwa.. mwanayanga mwenzetu manji amekaa pembeni..

Huwa nawaza sana hali hii ya kumtegemea mtu mmoja au kikundi cha watu wachache matajiri kuzamini na kuendesha timu itaisha lini ? nawaza tu siku manji akifariki, je tutaenda kumlilia mke wake kumuomba hela za mishahara hata kama yeye haipendi yanga au hapendi mpira?
ningependa sana kuona timu inaondoka huu mfumo wa kumtegemea mtu mmoja au wachache kiholela..


Maoni yangu mimi ni haya..

1. Yanga haifanikiwi na ni maskini sababu ya vipaumbele vya pesa na matumizi mabovu

hapa namaanisha timu ambayo haina kipato kikubwa imeajiri watu wengi sana ambao wanalipwa mishahara na posho ila role zao au majukumu yao hayana ulazima.. vyeo kama msemaji wa timu etc vingefutwa kupunguza gharama za mishahara msemaji wa timu anabaki kocha tu.. kama ulaya vile..

wangeitwa wataalamu , makampuni ya taaluma kama pwc, kpmg, delloite etc waje wathaminishe majukumu ya kila cheo.. kisha washauri role gani ziunganishwe na role gani zifutwe baada ya hapo kuwe na redundancy ya wasio na ulazima, na pia mishahara ipangwe kwa uhalisia..

2. Yanga haifanikiwi sababu ina poor marketing policy

hapa namaaisha yanga haijatangazi inavyotakiwa,, haitumii jina lake na mtaji wake wa mashabiki mamilioni kutengeneza pesa zake yenyewe.. mfano haina strong website, social network accounts, online tv etc... yanga ina uwezo wa kuwa na tv yake hata online tu kama millard hayo ambayo ingeendeshwa kisasa ingepata matangazo yake kama vodacom, tbl na makampuni binafsi, na bado kula hela za adsense ambazo zingeongeza mapato ya timu.. strong instagram accounts zingepost matangazo pia kama WCB wanavyofanya.. sitaki amini diamond ni smart than yanga management

3. ufatiliaji wa matumizi mabaya ya nembo na mauzo ya jezi feki ni mbovu

Hapa namaanisha mashabiki wengi wa yanga tunavaa jezi feki.. jezi zimejaa kariakoo na nchi nzima zina nembo za yanga ila ni feki... yanga haipati hata mia mauzo ya zile jezi feki.. unaenda taifa unakuta mashabiki wa yanga tumejaa kibao na njano na kijani zetu.. ila karibu wote tumevaa jezi feki ambazo club haijapata hata mia... kuwe na watu wa kufatilia wauzaji wa jezi feki na kuwashtaki na kwa kushirikiana na jeshi la polisi hii inawezekana kabisa ikiwekwa mfumo mzuri.. mauzo ya jezi yaifaidishe club..

4. Matumizi mabovu ya michango ya wanachama nayo ni sababu ya timu kulia ukata

wanachama tunalipia kadi kila mwaka, ila hela hizo hazieleweki zinaenda wapi... dunia ya sasa hela zinavunja uaminifu.. kuwe na mfumo rasmi wa kucontrol hela.. kila hela itoke kwa sababu.. hata kama ni 1000 tu au mia tano itoke kwa mbinde baada ya kuidhinishwa na ma signatories kibao...

hela ikiwa inatunzwa vizuri hii itashawishi hata mashabiki tukichangishwa tunatoa kwa moyo.. kuna wamachinga, wauza chips, boda boda, mama lishe wengi tu hawana kipato kikubwa ila wanaipenda sana yanga yetu,, kwamba ukimwambia arushe 1000 tigo pesa kuchangia timu yake yanga anatoa kwa amani kabisa.. ila sababu anajua kwa sasa hata nikitoa inaliwa na wezi viongozi na kulipana maposho hawezi kutoa kiurahisi...

mwenyekiti manji aliwahi kusema idadi ya mashabiki wa yanga ni kama milioni 35.. sina uhakika kama ni sahihi

Eti Yanga ina mashabiki 35 milioni!

sasa timu yenye mashabiki wengi hivyo inalia njaa.. si zaidi ya uchizi

timu yenye mashabiki wengi hivyo haijawai fika hata nusu fainali ya caf champions league.. kweli ujamaa umetulemaza.. yanga ni kubwa kuliko mazembe, kubwa kuliko enyimba, kubwa kuliko zanaco, kubwa kuliko APR sijui tumelogwa na nani


wanayanga wengine mnaruhusiwi kutoa maoni yenu.. Tunakosea wapi

Mimi yanga kwa jinsi navyoipenda hata kwa kukopa sishindwi ichangia buku buku kila mwezi.. kama tukiamua wanayanga tulipe mishahara ya wachezaji wenyewe kwa kuchanga.. ila sitachanga bila kuona mfumo rasmi wa kuzitunza hizi pesa za michango

by freshman aka Adam mwanayanga tawi la yanga Mabibo Hostel
 
Adam utafukuzwa wewe. Unaingilia dili za watu. Watu hawataki maendeleo wanataka ulwa.
 
Kula pongezi zangu mwanayanga unajielewa.
Yanga imepata bahati sana baada ya Simba kuingia katika mfumo mpya .
Wao wakijithaminisha na kujiuza kwa kuwashindanisha watu kiukweli na kujiuza kwa thamani yake sio kwa kushinikizwa na mtu au kikundi fulani.
 
Hizo hadithi tu. Badili mfumo sio kila siku kumtegemea mtu mmoja. Akisusa kama sasa bakuli zinatembea.
Yanga walipata bahati wakati Manji alipotaka kuikodisha.Ulikuwa sio mfumo sahihi lakini una afadhali kuliko kutembeza michango.
Simba wamepata bahati ya kumpata mwekezaji anayeipenda timu yao.
Kuwapata wawekezaji wa kuwashindanisha ni wishfull thinking. Sio jambo rahisi kihivyo.
 
Tatizo serikali...Toka enzi za Yanga kampuni na Yanga Bomba...ingekuwa level za TP Mazembe,Esperance nk...Mzee Akilimali aliongelea vizuri kwenye kipindi cha Baruani...viongozi ndio hawataki huo mfumo mpya..cha kufanya bakora zipigwe hakuna namna...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…