Kama kweli Mungu yupo kwanini ameruhusu wanadamu kuteseka?

Kama kweli Mungu yupo kwanini ameruhusu wanadamu kuteseka?

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Hoja Za Mungu ni ngumu kuelewa ila pia ni nyepesi kuelewa ukitumia akili vizuri sana

Let me go straight to the topic

Kwanini Mungu ameruhusu wanadamu kuteseka? Ukweli ni kwamba Mungu Hajaruhusu mwanadamu kuteseka ila mwanadamu anajitesa mwenyewe

Katika maandiko ya Biblia inasema Mungu alimuumba mwanadamu na akili nyingi kuliko hata malaika

kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. Wakasema: Subhanaka, Wewe umetakasika! Hatuna ujuzi isipokuwa kwa uliyo tufunza Wewe. Hakika Wewe ndiye Mjuzi Mwenye hikima.’” (Kurani 2:31-32)

Mungu akamgeukia Adam na kusema:

“‘Akasema: Ewe Adamu! Waambie majina yake. Basi alipo waambia majina yake alisema: Sikukwambieni kwamba Mimi ninajua siri za mbinguni na za duniani, na ninayajua mnayo yadhihirisha na mliyo kuwa mnayaficha?” (Kurani 2:33)

Kwahiyo mwanadamu ni kiumbe ambacho Kulikuwa kikamilifu zaidi ya Viumbe vyote vya mwenyezi Mungu
Na mwanadamu Alitakiwa kusujudiwa na viumbe vingine vyote apa chini na juu ya dunia
Kwasababu mwanadamu ametokana na Mungu mwenyewe

Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo. Na nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayo tokana nami, basi muangukieni kwa kumt'ii.” (Kurani 38:71-72)

Mwanadamu ni tofauti na viumbe vingine vya Mungu mwanadamu Kulikuwa kiumbe pendwa kwa Mungu
Kwanini Mungu aliruhusu mwanadamu kiteseka ? Ni pale mwanadamu alipokosa kutii maneno ya Mungu

Mwanzo 2:17
“lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.”

‭‭
hapo adamu alipewa maagizo ya Mungu na Mungu alimuamini adamu kwasababu alijua adamu ni kiumbe kikamilifu ndo maana alimpa maagizo.

Adabu kwa upumbavu wake akakosa kitii maneno ya Mungu akatii maneno ya mke wake na pia mke wake alikosa kutii maneno ya Mungu akatii ya shetani Mungu akalaani

Mwanzo 3:15-17
“Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.

Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;”
 
Msipokazana kufanya kazi kwa jasho na kutumia maarifa vichwani mwenu mtahoji sana uwepo wa Mungu.

Uvivu na ujanja ujanja vinawaandama watu vijana kufanya kazi ngumu hawataki badala watoke kuhangaika wanajifungia vyumbani kusoma vi-article vilivyoandikwa na jobless wenzao wakati wakiwa down kuhoji uwepo wa Mungu na kudhani Mungu kuwepo au kutokuwepo kunawafanya wawe walivyo wasijue kisababishi ni uvivu wao
 
Mungu hatesi wanadamu bana
maagano mliyoingia na mababu na mabibi zenu ya kumwaga damu za wanyama halafu hamuwaulizi maana yake nini! ndiyo yanawatesa kizazi hadi kizazi.
maandiko matakatifu yanasema asiwepo mtu yeyote ambaye anafata mambo ya uganga, mizimu, uchawi,n.k kwa maana mambo hayo ni chukizo kwake.
jina la Mungu ni ngome imara anayelikimbilia ataondokana na mateso yanayosababishwa na mila za kwenu.
 
Mimi kwa maoni yangu ni kwamba mateso yanayowapata mwanadamu Mungu mwenyewe ameruhusu na anayakubali.
Point yangu ni hii,
Mfano, ikiwa kuna jambo lolote baya linakwenda kuwatokea watu na litawaumiza sana na una uwezo wa kulizuia lisitokee ila ukaliacha likatokea na likaumiza watu ni wazi kwamba na wewe umehusika kuwaumiza.
Najua hapo unaweza kumtetea Mungu kwamba huwa anatoa onyo kwanza Kisha ukikaidi ndo unaangukia kwenye matatizo. Hilo nalipinga kwa hoja hii,
Mfano, we mjuzi sana wa magari na unaona kabisa gari inataka kuanza safari na unaona kuna hitilafu inayoweza kusababisha ajali unawaonya walitatue kwanza hilo tatizo la gari yao ndo waanze safari wanaleta ubishi, wewe uwezo wa kusaidia unao. Je utaacha kuwatengenezea ili uwanusuru na ajali au utaacha ili baadae litakalowakuta useme "nilisema mimi na hamkunisikia" ??
Ikiwa unawapenda utawatulia tatizo lao hata kama wanaleta ubishi, ikiwa huwapendi utaacha tu na liwakute lolote.

Kama mfano wangu hapo umekuchanganya naomba nirudi kwenye mada. Umesema Mungu alimuagiza Adam asile tunda na Adam akala, ni wazi kwamba Mungu alijua kwamba Adam atakula, kwa hiyo wakati Mungu anatoa agizo hilo ni kwamba akaandaa na adhabu kabisa kwa sababu alijua Adam hatatii hilo agizo.

Ikiwa Mungu alimpa Adam agizo na anajua hatatii kisha anampa adhabu ya kutotii ni wazi kwamba Mungu hakuwa akimpenda Adam na alikuwa anatafuta tu sababu ya kumuadhibu.

Hata wewe hapo ikiwa una uwezo wa kutatua shida za watu na huzitatui hilo halipingiki kwamba umekubali na unahusika na mateso yao
 
Ni michakato tu ni kama kukua, ukuaji.

Imeumbwa hivyo ili tu mabadiliko yawepo so muda uwepo so kila kitu kiwepo.

Usiyakatae mabadiliko kutoka hali moja kwenda nyingine, hiyo unayoita hali nzuri au mbaya ni hali tu inayobadilika na kukuwezesha wewe kuwepo.

Kila kitu kikiwa sawa watu watajitungia mateso ambayo hukuwahi kuyawazia. Mfano watoto watalalamika kuwa ni mateso kuwa mtoto kwa nini Mungu hakutuumba kama watu wazima kamilifu ili tusihangaike kukua tena. Kwani hakuweza hivyo?

Amin aamin nakuambia, hata suala la umasikini na utajiri ni hivyohivyo, utofauti unaruhusu michakato na ndio inatokeza muda na ndio unatokeza uwepo. Enjoy
 
Mimi kwa maoni yangu ni kwamba mateso yanayowapata mwanadamu Mungu mwenyewe ameruhusu na anayakubali.
Point yangu ni hii,
Mfano, ikiwa kuna jambo lolote baya linakwenda kuwatokea watu na litawaumiza sana na una uwezo wa kulizuia lisitokee ila ukaliacha likatokea na likaumiza watu ni wazi kwamba na wewe umehusika kuwaumiza.
Najua hapo unaweza kumtetea Mungu kwamba huwa anatoa onyo kwanza Kisha ukikaidi ndo unaangukia kwenye matatizo. Hilo nalipinga kwa hoja hii,
Mfano, we mjuzi sana wa magari na unaona kabisa gari inataka kuanza safari na unaona kuna hitilafu inayoweza kusababisha ajali unawaonya walitatue kwanza hilo tatizo la gari yao ndo waanze safari wanaleta ubishi, wewe uwezo wa kusaidia unao. Je utaacha kuwatengenezea ili uwanusuru na ajali au utaacha ili baadae litakalowakuta useme "nilisema mimi na hamkunisikia" ??
Ikiwa unawapenda utawatulia tatizo lao hata kama wanaleta ubishi, ikiwa huwapendi utaacha tu na liwakute lolote.

Kama mfano wangu hapo umekuchanganya naomba nirudi kwenye mada. Umesema Mungu alimuagiza Adam asile tunda na Adam akala, ni wazi kwamba Mungu alijua kwamba Adam atakula, kwa hiyo wakati Mungu anatoa agizo hilo ni kwamba akaandaa na adhabu kabisa kwa sababu alijua Adam hatatii hilo agizo.

Ikiwa Mungu alimpa Adam agizo na anajua hatatii kisha anampa adhabu ya kutotii ni wazi kwamba Mungu hakuwa akimpenda Adam na alikuwa anatafuta tu sababu ya kumuadhibu.

Hata wewe hapo ikiwa una uwezo wa kutatua shida za watu na huzitatui hilo halipingiki kwamba umekubali na unahusika na mateso yao
Kama umesoma hoja mada yangu vizuri nakuelewa huwezi kutoa hoja hizi au mada hii kwasababu gani Kwasababu Mungu alipo muumba adamu akambariki na akili nyingi kuliko viumbe vyote chini na juu ya dunia
Akampa akili ya kujua wema na ubaya
Na Adam alipotenda kosa lile sio kwamba hakujua kuwa ni kosa alijua ni kosa aka fanya kwa kutokuheshimu Mungu
 
Hivi ilikuwa kuwaje tukawa tunaongea lugha tofauti tofauti ilihali wote tumetokea kwa mtu mmoja? Je majina ya vitu na wanyama au nayetu sisi unaweza kujua chanzo chake.
 
Kama umesoma hoja mada yangu vizuri nakuelewa huwezi kutoa hoja hizi au mada hii kwasababu gani Kwasababu Mungu alipo muumba adamu akambariki na akili nyingi kuliko viumbe vyote chini na juu ya dunia
Akampa akili ya kujua wema na ubaya
Na Adam alipotenda kosa lile sio kwamba hakujua kuwa ni kosa alijua ni kosa aka fanya kwa kutokuheshimu Mungu
Nakubaliana na wewe kwamba Adam alipewa akili nyingi na alilolifanya alijua kufanya vile ni kutokumheshimu Mungu, swali langu kwako, je Mungu alijua kwamba Adam hatatii hilo agizo? Ikiwa alijua ni wazi kwamba alishaandaa na adhabu kabisa. Na hapo ndo inaonyesha hakuwa na upendo kwa Adam.
 
Back
Top Bottom