Opportunity Cost
JF-Expert Member
- Dec 10, 2020
- 9,034
- 6,913
Heshima Sana kwenu wadau.
Moja kwa moja kwenye mada, kumekuwa na dhana mbalimbali kwamba nchi nyingi za Afrika Magharibi ni Maskini na Zina migogoro mingi ya waasi na kisiasa kuliko nchi za ukanda mwingine hasa Sadc
Lakini cha kushangaza hizo nchi zinazoitwa maskini, zenye migogoro na zenye GDP ndogo ndio mara kwa mara zinaandaa mashindano ya Caf kama CHAN, Afcon nk nk na zinabadilishana na nchi za Kiarabu.
Ukiangalia viwanja vyao mfano Cameroon na Gabon unakuta Wana viwanja vingi na vizuri sasa Hawa wanawezaje wakati Nchi zinazoitwa kubwa na zilizoendelea kama Kenya, Tanzania, Angola, Zimbabwe nk zinashindwa kuwa wenyeji wa mashindano mbalimbali ya Soka kama West Afrika?
Hapa nahisi huwa tunapigwa changa la macho maana wanaoitwa maskini wako vizuri na wanafanya makubwa na wanaoitwa Wameendelea ndio hamna kitu,nataka kufahamu Tanzania tunakwama wapi wakati kimaendeleo tunaaminishwa kuwazidi hao wa huko?