Kama kweli nchi za Gabon, Cameroon na Congo Brazavile ni maskini zinawezaje kuandaa mashindano makubwa ya Soka Afrika kushinda Tanzania?

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
9,034
Reaction score
6,913
Heshima Sana kwenu wadau.

Moja kwa moja kwenye mada, kumekuwa na dhana mbalimbali kwamba nchi nyingi za Afrika Magharibi ni Maskini na Zina migogoro mingi ya waasi na kisiasa kuliko nchi za ukanda mwingine hasa Sadc

Lakini cha kushangaza hizo nchi zinazoitwa maskini, zenye migogoro na zenye GDP ndogo ndio mara kwa mara zinaandaa mashindano ya Caf kama CHAN, Afcon nk nk na zinabadilishana na nchi za Kiarabu.

Ukiangalia viwanja vyao mfano Cameroon na Gabon unakuta Wana viwanja vingi na vizuri sasa Hawa wanawezaje wakati Nchi zinazoitwa kubwa na zilizoendelea kama Kenya, Tanzania, Angola, Zimbabwe nk zinashindwa kuwa wenyeji wa mashindano mbalimbali ya Soka kama West Afrika?

Hapa nahisi huwa tunapigwa changa la macho maana wanaoitwa maskini wako vizuri na wanafanya makubwa na wanaoitwa Wameendelea ndio hamna kitu,nataka kufahamu Tanzania tunakwama wapi wakati kimaendeleo tunaaminishwa kuwazidi hao wa huko?
 
Africa magharibi wamewezekeza sana kwenye soka viwanja vizuri, academy za michezo n.k kwahyo inakuwa rahis sana kuhost hayo mashindano,hivyo pesa za kujiandaa na mashindano zikitoka CAF wanafanya tu marekebisho ya viwanja vyao.Kwahyo tukja huku bongo tuna viwanja viwili vzur ambavyo vipo mkoa mmoja hvyo inakuwa ngumu kuhost mashindano makubwa hapa cha msingi ni kuishauri serikali ijenge viwanja vizuri kama kle cha Dar angalau mikoa mitano na vidogo vidogo kama karume na JK.

Naamini tukiomba kuhost hayo mashindano tutapata, Pia wenzetu hawaoni hasara kuwapeleka wale wenye vipaj huko ulaya ili wakajifunze vizuri na hatimaye nchi kupata team bora ya taifa bt kwa huku kwetu hata ukiwa na kipaji serikali wala haina time na wewe labda kwenu uwe mambo Safi unawweza endeleza hyo kipaji .

Tff wapo kwenye kula pesa tu team ya taifa unakuta inakaa kambi siku tatu kisha mechi.
 
Hao Wana strategy nzuri maana sisi bongo sijui akili ziliendaga wapi,ukiangalia west africa wamewekeza Soka kama ajira kwa watu wao na mapato ya fedha za kigeni kwa wanamichezo wao walioko abroad kutuma pesa kwao yaani remittances

Huku Bongo kama ishu ya mpira kwa maana ya kuibua vipaji imetushinda Basi tujenge viwanja vizuri na tuiboost ligi ya ndani Ili ivutie wawekezaji na wachezaji wa kigeni tupate kodi kama ilivyo ligi ya England.

Pia ishu za bongofleva zinaeeza kututoa maana kwa Sasa hakuna kitu tunaweza jivunia kuwa smart
 
Ni focus tu
 
Naomba serikalini iwekeze viwanja hata vya watazamaji 30,000 vipya mikoa ifuatayo
1. Mwanza
2. Arusha
3. Dodoma
4. Mbeya
5 Morogoro

Tukipata hivyo na vilivyopo Zanzibar na Dsm vinakuwa 8 ambavyo vina standards nzuri.
Hapo hata World Cup tunaomba
 
Tumuombe Mo tufanyie kule Mo Arena Xtra.
 
Nadhani EA ishirikiane Tanzania, Kenya na Uganda ziungane kuandaa mashindano kwa pamoja. Kama ilivyokuwa Gabon na Equatorial Guinea.
 
Hizo nchi pia zimeshawahi kucheza mashindano ya kombe la dunia idhan kama ni maskini kutushinda.
 
Hizo nchi pia zimeshawahi kucheza mashindano ya kombe la dunia idhan kama ni maskini kutushinda.
Mpira hauhusiani na utajiri mkuu, ingekuwa hivyo USA na China ndo zingekuwa zinatesa kwenye soka na sio Brazil.

Shida ni kwa nchi zetu za EA hususan Tz huwa tunakosa viongozi wa mpira, huwa wanahonga ndo wanachukua ofisi, mfano rais wa tff ilikuwaje akawa Wallace Karia na sio Aly Mayai Tembele? Ni kwmb Karia alipita kirushwa rushwa na ndiyo maana mpk leo tunasua sua.

Kuhusu kuandaa mashindano sio kweli kwamba hatuna viwanja vya kuruhusu mashindano makubwa ya kiafrika, tuna viwanja vingi vzr hata kuzidi nchi nyingi, angalia ligi yetu tu ambayo cku hz mechi nyingi tunaziona live, viwanja vingi tu vzr.

Tatizo ni viongozi na sio ukosefu wa viwanja, tungekuwa na viongozi walio commited kwnz kabisa wangeumwa na kushindwa kuandaa mashindano makubwa kwa nchi inayopenda soka km Tz, wangehakikisha wanaacha legacy yao kwa kuhakikisha nchi inaandaa mashindano makubwa but kinyume chake viongozi wengi wa michezo nchini wanaingia ofisini kwa lengo la kupiga pesa na sio kuacha alama kwakuwa sio wanamichezo na hawaumwi na mwenendo mby wa michezo nchini.


Hivi mpk leo timu yetu ya taifa kila siku inatuaibisha tu lkn hatusikii kauli za kishujaa toka kwa viongozi km kina Karia yote hyo ni kwasababu sio wanamichezo so hawaumwi kabisa na mwenendo mbovu, nchi mpk leo haina ligi ya kueleweka ya watoto, tm kubwa km Simba na Yanga hazina academy za kueleweka lkn kina Karia kwasababu sio wanamichezo hawaoni umuhimu wa kuzilazimisha hizi timu ziwe na academy.

Nimeandika walaka mrefu cz ni jambo linalokera sn kuona vinchi maskini kabisa vya Africa vinaandaa michuano mikubwa lkn nchi zenye afadhali zimekaa tu eti kisa hatujui mpira (hii ndiyo mentality ya viongozi wetu) but ukweli ni kwamba tunaweza kuandaa na tuna viwanja vingi tu vzr na vinavyofaa kuliko hata viwanja vya baadhi ya hizo nchi zinazoandaa.
 
 
 

Iondoe Gabon kwenye hyo list coz Wana hela kufuru za mafuta
 

Wanasiasa nuksi Sana!

Wanageuza viwanja vya mitaani kuwa gereji bubu

Halafu wakisimama majukwaani wanajifanya wanasapoti michezo

Unafiki mtupu
 
Kwa hiyo kuhost ligi za mchangani Afcon na Chan kwako ndio kunakufanya uone hizi nchi ni tajiri si ndio ?

Ama kweli watu mmerogwa sijui na Nani ?
 
Bro taja kwanza hivyo so called "Viwanja vingi vizuri kupita nchi nyingi tu"..? Usidanganywe na Camera za Azam.
 
Tunaweza tu kuandaa ndondo kapu
 
Kila kitu mnatolea mfano USA wakati unafahamu USA inatamba kwenye mchezo gani na china inatamba kwenye eneo lipi. Sie hatuna eneo lolote tunalotamba iwe kwenye madini ,utaliii,movies,mpira etc.

Masuala ya kuandika gazeti reeefu kisa USA na china hazitambi kwenye soka its useless point wakati unaona kabisa ubabe USA ulipo kwa utajiri wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…