Kama kweli viongozi Simba mmetuma maombi TFF wasogeze mbele mechi dhidi ya Yanga mnatuaibisha

Pettymagambo

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2017
Posts
1,490
Reaction score
8,227
Kwahii taarifa inayotrend ya viongozi wa Simba eti kutaka game dhidi ya Yanga isogezwe mbele kisa tu kuwepo kwa mechi ngumu wiki moja, yaani siku 7 mbele dhidi ya Bingwa Mtetezi wa Champions League.

Mjue mnatufanya mashabiki wenu wanyonge na tuonekane tunawaogopa hawa Yanga.

Lakini pia kama game na Yanga itaahirishwa maana yake kutakuwa na siku 12 za Simba kukaa bila kucheza mechi kutoka tarehe 10 ya mechi na Ihefu mpaka 22 dhidi ya Wydad. Je, hamuoni kama timu itakaa muda mrefu?

Viongozi wetu mtambue Yanga nao wana mechi kama sisi kimataifa pia, tena wao baada ya derby watasafiri kwenda Nigeria, lakini sisi ambao tutakuwa na mechi hapahapa eti ndo tuombe Derby isogezwe mbele?

Mnatufanya wanyonge mbele ya Yanga, yaani kama vipi TFF msikubali ombi hili, na kama ni kuburuzwa na Yanga na tuburuzwe tu na sio mechi isogezwe mbele.

Tunaonekana wanyonge kwa Yanga.
 
Kama ni kweli nawaunga mkono, mana mechi dhidi ya Waydad ni ngumu zaidi na Simba inahitaji kupata ushindi mnono ili kujihakikishia kwenda nus fainali za Caf. Yanga hata ikifungwa na simba bado bingwa atabaki kuwa ni Yanga tu. Haita athiri ubingwa wa Yanga

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mechi ya simba vs Yanga ni kulinda heshima tu Maana ubingwa kwa asilimia kubwa ni wa Yanga .
Zaidi itaenda kutuongezea majeruhi tu ndani ya kikosi.
 
na si ajabu hata waganga wao wamehusika kuwashauri juu ya hili swala,mangungu anatuaibisha
 
Washaanza visingizio eti Inonga kaumia mechi ya jana ,sasa huyo Kennedy na yule Msudan mmewasajili wafanye kazi gani.
 
Simba wanaogopa vipigo mfululizo. Maana mechi na Ihefu, watafungwa! Na ile vs Yanga, watafungwa! Wakija Waarabu, nao wanawashushia kipigo! Nusu fainali vs Azam Fc, kipigo! Maana wachezaji ni wale wale kila mechi!

Furaha ya ushindi kwao ilitamatika siku ya jana, baada ya Ihefu kuamua kuweka mpira kwapani, na hivyo kuwekeza nguvu kubwa kwenye mechi yao ya ligi kuu, kule Mbarali.
 
na si ajabu hata waganga wao wamehusika kuwashauri juu ya hili swala,mangungu anatuaibisha
Tunachekwa na kuzomewa tunataka kukacha mechi, kwanza kunatofauti ya siku 7 kati ya mechi dhidi ya uto na mwarabu, sasa mie sioni sababu ya kuomba game isogezwe mbele, yaani kama vipi kipigwe tu.
 
Yanga mbona mnaweweseka kama changudoa aliyetoa mimba?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Wewe utaiota Simba sana hadi utaokota makopo,unaitaja Simba kama ndiyo ibada yako.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kwann unaleta habari ambazo huna hakika nazo.
 
we punguani kweli.... huna uhakika wa taarifa unayoitoa then unajifanya kutiririsha mchozi hapa....koma kabisa!! "chura wa Jangwani weee!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…