matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Luka 19:17
Akamwambia, Vema, mtumwa mwema; kwa vile ulivyokuwa mwaminifu katika neno lililo dogo, uwe na mamlaka juu ya miji kumi.
Kuna uhusiano wa uwezo wa uongozi, na uwezo wa kuzalisha faida kwenye maisha ya kila siku. Mtu ambaye anauwezo wa kupewa elfu 10 ndani ya siku akakuletea 13000 ndiye anaqualify kuongoza kwa Mujibu wa Yesu.
Yule jamaa aliyezalisha zaidi alipoleta hesabu , Zawadi yake ilikuwa ni kutawala au kuwa kiongozi.
Lissu anaingia akiwa na sura ya umasikini lakini akiwa hana historia ya uzalishaji. Sijajua kupitia uanasheria wake umeweza kumfanya azalishe kiasi gani kama ushahidi wa uwezo wake wa kumonetize ujuzi wake ili Yesu amfanye mtawala bora hapo chadema.
Lakini kama ni hivihivi tu, atapata shida kuliko tunavyodhani. Nampenda na namuunga mkono ila hilo nalo alijue.
Viongozi wa kiafrika wenye poverty mentality wasioweza kuzalisha kwa ajili yao na kuwa na akiba kwa ajili ya kusaidia jamii ndio wanakuwa wezi wanapoingia madarakani. Wanajilimbikizia mali na kutengeneza magenge ya wizi serikalini na kwenye jamii maana wanaamini hawana uwezo wa kuzipata hizo kwa nguvu zao.
Ni hilo tu.
Mtumishi Matunduizi.
WWasalam