Kama Lissu Mgonjwa kwanini anahangaika?

Kama Lissu Mgonjwa kwanini anahangaika?

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Kwa mara ya kwanza CHADEMA imekubali kwamba Tundu Lissu ni mgonjwa na anatumia dawa.

Wamekubali hili baada ya Lissu kukamatwa na kukaa saa 24 bila kutumia dawa zake.

Inakuwaje mtu huyu ambaye ni mgonjwa anayerudi nchini Ubelgiji mara kwa mara kupata matibabu mnamtanguliza mbele katika jambo (unlawfull assembly) ambalo mnajua fika litamuingiza kwenye matatizo?

Soma Pia: Lissu, Mnyika na Sugu wakamatwa na Polisi usiku huu. Baadhi ya Waandishi wa habari pia wakamatwa

Huu ni ubinafsi wa hali ya juu. Hii ina tofauti gani na kutaka kummaliza ninyi wenyewe? Acheni ubinafsi na kuweni na huruma.

Huyu mtu ana matibabu makubwa bado hajamaliza. Msaidieni Lissu apone badala ya kumtumia. Matibabu yake yanahitaji utulivu.
 
Mashetani wageuka wenye huruma!

Ukweli ni kwamba, nafsi zinawasuta kwa ujambazi mliowafanyia Lissu na wenzake. Kama wan maakosa ya kijinai, walitakiwa wakamatwe na washitakiwe, ila mnajua hawana kosa la aina yoyote zaidi ya uharamia wenu.

Mtateseka sana nyie mashetani wenye umbo la binadamu na mtakufa kama lile dhalimu lingine liliokuwa katili kwa wapinzani Mungun akaamua kulitanguliza.
 
Mmmmh..yaani mtu akiwa na changamoto ya afya,endelevu ya kawaida haruhusiwi kufanya kazi?..au mimi ndio sijaelewa??
 
Jirani yangu mmoja ni msomi kwelikweli....kila hafla za dini anapewa KIPAZA SAUTI atupe naswaha....kwa kuwa pia anatumia dawa ziitwazo HALOPERIDOL kutoka pale wodi nambari 14 Mirembe hospitali bado wafuasi wake hawaamini kuwa anao ugonjwa huo...katika hafla ya maulid ya juzi baada ya tu kupewa KIPAZA SAUTI akaivua kanzu yake ya Oman na kutupa kilemba chake chini halafu akatoka mbio mkononi akiwa na "MIC"....ilikuwa hamkani hali si shwari,ila mwishowe pilau tukalila....

#Nchi Kwanza[emoji2956]
 
Back
Top Bottom