Kama Makocha watatu wazalendo wanaweza kutufanyia vile dhidi ya Ethiopia, basi CCM ni noma

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
1,213
Reaction score
1,918
Hakika lililofanywa na makocha wetu wa Taifa Stars Moroko, Mgunda na Julio ni kutupotezea muda na kutoheshimu hisia zetu.

Kwahiyo Mgunda na Julio ndo wamemshauri Moroko kuwa Novatus na Mao wanaweza kucheza namba 6 na 8 na tukaweza kuwa na kiungo kinachonyambuka, kwamba Kibabage anaweza kucheza winga ya kushoto namba 11 na timu ikawa vizuri kwenye transition na kupiga cross au ku-cut in kwamba Balua yuko vizuri kwenye Flanks kuliko Mzize?

Yaani Taifa Stars ya sasa inacheza nyumbani Uwanja wa Benjamini Mkapa tena dhidi ya Ethiopia ikiwa na wachezaji 8 wa kuzuia na 3 ndo wa kushambulia kweli?

Kila mchezaji anajichezea kivyake hakuna hata muunganiko unaonekana, kila mchezaji anajichezea tu anavyoweza.

Kifupi pale uwanjani kulikuwa na kikundi cha wahuni kimeenda kupiga ndondo bila kocha.

Hakika CCM ni noma maana toka tupate UHURU ndo kitu pekee ambacho kimefaulu kuishi kwenye nyakati tofauti kuliko kitu chochote cha kijumuiya kwenye nchi yetu.

Kama tukiweza kukopi kinachoifanya CCM iweze kudumu halafu tuka-apply kwenye kila kitu tunachofanya kama nchi tutafika mbali kama nchi.
 
Benchi la ufundi linabahatisha halina ujuzi halina uwezo
 
Kukopi hapo ilikuwa ni kuzima taa za taifa mzize anapewa mpira zikiwaka uko kwenye nyavu ya Ethiopia basi ushindi
Sema Sasa caf hawataelewa
 
Hakika lililofanywa na makocha wetu wa Taifa Stars Moroko, Mgunda na Julio ni kutupotezea muda na kutoheshimu hisia zetu.

Kwahiyo Mgunda na Julio ndo wamemshauri Moroko kuwa Novatus na Mao wanaweza kucheza namba 6 na 8 na tukaweza kuwa na kiungo kinachonyambuka, kwamba Kibabage anaweza kucheza winga ya kushoto namba 11 na timu ikawa vizuri kwenye transition na kupiga cross au ku-cut in kwamba Balua yuko vizuri kwenye Flanks kuliko Mzize?

Yaani Taifa Stars ya sasa inacheza nyumbani Uwanja wa Benjamini Mkapa tena dhidi ya Ethiopia ikiwa na wachezaji 8 wa kuzuia na 3 ndo wa kushambulia kweli?

Kila mchezaji anajichezea kivyake hakuna hata muunganiko unaonekana, kila mchezaji anajichezea tu anavyoweza.

Kifupi pale uwanjani kulikuwa na kikundi cha wahuni kimeenda kupiga ndondo bila kocha.

Hakika CCM ni noma maana toka tupate UHURU ndo kitu pekee ambacho kimefaulu kuishi kwenye nyakati tofauti kuliko kitu chochote cha kijumuiya kwenye nchi yetu.

Kama tukiweza kukopi kinachoifanya CCM iweze kudumu halafu tuka-apply kwenye kila kitu tunachofanya kama nchi tutafika mbali kama nchi.
KATIBU AACHIE NGAZI HARAKA SANA.
 
Back
Top Bottom