Kama masihara masihara hivi kumbe ndo tunazeeka taratibu

Kama masihara masihara hivi kumbe ndo tunazeeka taratibu

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Tukiwa humu humu JF tukichaluana kwa hoja, January hadi December! Uchaguzi hadi uchaguzi!

Ulianza ukiwa na umri mdogo, Mara paap 35, 40, 45 ,50..... n.k ndo zinasogea hivi kama masihara!

Uzee usikieni tu, maisha ya upweke watoto wakiwa mbali!

TUJIPANGE WADAU
 
Mimi huu mwaka sihuhesabii katika Umri wangu.. 2020 Mwaka mbaya Tokea January hadi leo Nov..

ikibidi acha kuhesabu miaka kabisa kama saddam Hussein,hakutaka kuzeeka akaamua aache kuhesabu miaka yake alipofika 60[emoji23] na birthday party akaacha kufanya
 
Tukiwa humu humu JF tukichaluana kwa hoja, January hadi December! Uchaguzi hadi uchaguzi!

Ulianza ukiwa na umri mdogo, Mara paap 35, 40, 45 ,50..... n.k ndo zinasogea hivi kama masihara!

Uzee usikieni tu, maisha ya upweke watoto wakiwa mbali!

TUJIPANGE WADAU
Maisha ya Mwanadamu Ni mafupi Sana Jamani...Hatujui siku Wala saa.. Japo Mimi Sio mtakatifu...nawakumbusha kumrudia Mungu..

Yaaani Miaka inakimbia na umri haurudi nyuma
 
Ila najiona kabisa nazeeka na utamu wangu kwenye fimboya musa...😎😎
 
Nimekusoma vizuri mjomba... yaani sisi wa under 30 badobado uzee[emoji38]
 
Nimekusoma vizuri mjomba... yaani sisi wa under 30 badobado uzee[emoji38]
Mkuuu...nakwambia umri hauchelewi... Siku utashangaa um30 hi hapa. Ukiangalia nyuma Ni MAJUTO TU ..

Utumie umri wako vizuri.. Tena Sana especially ujana wako..achana na dhana kuwa wanaume hawazeeki..
 
Aisee yaaani..Siku zinasonga..usiku mchana usiku mchana...Ukijakuangalia ushakuwa mtu mzima KABISAA...
[emoji3][emoji3][emoji3].....Mimi najiona nishakuwa mtu mzima Sasa.
Sio siri mimi naogopa kuzeeka,Yaani hua nikiona wazee hawana nguvu, ngozi imesnyaaa.Nachoka mnoo [emoji2297][emoji2297][emoji2297]
 
Uzee uja bila hiar!!!

Daaa Kiutani utani nina ¼ Robo karne sahiv daa(25)

Afu ukichek mchezo bado sijaulewa...nimevaa jez tu:
 
Kweli mkuu, nilifikiri jambo nikaona bora nijenge nyumba simple ya kisasa. Huko mbeleni watoto wakisepa na Mungu akatujalia kuuona uzee na mwenzangu upweke utakuwa si mkubwa kama ningekuwa na bonge la jumba.
 
Si Mchezo!!!!Miaka Takribani Saba Tangu Naifahamu JF!!
 
Back
Top Bottom