Kama maskhara, Simba inapangiwa na yanga nini cha kufanya na wanatekeleza

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Kama utani lakini inatokea.Ninaona yanga wanafanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa wachezaji wa Simba na viongozi waliopo.

Siamini kabisa kuhusu matukio mengi yaliyotokea hasa kupitia kwa wachezaji wa kigeni kama yalikuwa bahati mbaya.

Baadhi ya wachezaji walilipwa na yanga kucheza chini ya kiwango.Wa kwanza ni Inonga.

Nilitarajia kuwa Simba wangewaacha wachezaji wengi pro bila kujali chochote lakini ni masikitiko yangu kila wanalopangiwa na yanga wanalifanya.

Tulipangiwa kucheza shirikisho na ukweli uko wazi kwa hili kutokea.
Tulipangiwa kufungwa tano,na mtu anasema mapema kabisa eti ameoteshwa na kweli inatokea.Hii si bahati mbaya.

Tumeshaambiwa bado miaka miwili hatutachukua ubingwa na dalili zimeanza kujionyesha iwapo viongozi tulio nao ndio hawa hawa.Tunaona machawa walivyopangwa kuwatetea eti tusiwaseme viongozi wetu!

Tunaona uwepo wa Mo ni kwa ajili ya kuifanya Simba iwe timu machachari kama KMC lakini ukweli haina malengo ya kwenda popote Africa.Usajili wa Chama ni dalili kuwa hawana mpango wa kuleta mbadala wa chama.

Simba itaendelea kuishi kwa kuchechemea na kupigania nafasi ya pili au ya tatu hadi viongozi kama mangungo waondoke,wafadhili kama mo aachane na Simba.Kama Singida na Ihefu wanapata wafadhili,itakuwa Simba?
 
Haya ni maneno ya kujifariji tu...ukweli ni kwamba Yanga imeimarika zaidi kuliko Simba na ndio sababu imeweza kuchukua ubingwa misimu mitatu mfululizo....kama Simba itaendelea kuamini hizi sababu za kishabiki msimu ujao itaishia nafasi ya tatu mapema zaidi kuliko msimu huu,,Azam FC nao taratibu wameshaanza kujipata.

Simba ilipochukua ubingwa misimu minne mfululizo ilikua na ubora huu huu ilionao sasa isipokua yanga na timu nyingi katika ligi zilikua dhoful hali..baada ya udhamini wa AzamTV,,timu nyingi ziliimarika na timu ya yanga iliimarika zaidi kwenye wadhamini, uongozi, wachezaji na utaalam wa uendeshaji wa soka walioupata Laliga..

Ili Simba ifanye vizuri zaidi msimu ujao na mingine inabidi ifanye mageuzi kwenye uongozi sio lazima wabadilishe watu ila waliopo wabadilike kifikra na kuwajibika kwa kuendesha soka kitaalam na sio kishabiki,,, hakuna ubaya hata wakituma viongozi wao kwenye klabu ya wanachama inayofanya vizuri duniani wakajifunza,,kama Real Madrid..
 
kwa kumuongeza chama Mshahara na mwaka moja with options ya 2 years kuna shida
 
Nilishangaa viongozi wa Simba kuhangaika na mkataba wa Kibu, Sasa hv wanahangaika na Mzamiru. Ni Kama wakati wa kumuongezea mkataba shabalala badala ya kujikita kutafuta mbadala wake wao wanawekeza pesa nyingi kwa mtu aliye na umri mkubwa.
Mo Hana uwezo zaidi ya kunitumia Simba kujiongezeaa umaarufu na mapato.
Mchakato wa uwekezaji wa Simba ulikuwa mchakato wa hovyo kabisa

.
 
Nasikia kelele Hamisa,Hamisa.....!

Sijui kafanyaje? Hivi Aziz Ki bado Kuoa ee!

Kama keshaoa aache mara moja hiyo michezo Vitoto vya Bongo vina UTI kali.?
 
Kama utani lakini inatokea.Ninaona yanga wanafanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa kwa wachezaji wa Simba na viongozi waliopo.

Siamini kabisa kuhusu matukio mengi yaliyotokea hasa kupitia kwa wachezaji wa kigeni kama yalikuwa bahati mbaya.

Baadhi ya wachezaji walilipwa na yanga kucheza chini ya kiwango.Wa kwanza ni Inonga.

Nilitarajia kuwa Simba wangewaacha wachezaji wengi pro bila kujali chochote lakini ni masikitiko yangu kila wanalopangiwa na yanga wanalifanya.

Tulipangiwa kucheza shirikisho na ukweli uko wazi kwa hili kutokea.
Tulipangiwa kufungwa tano,na mtu anasema mapema kabisa eti ameoteshwa na kweli inatokea.Hii si bahati mbaya.

Tumeshaambiwa bado miaka miwili hatutachukua ubingwa na dalili zimeanza kujionyesha iwapo viongozi tulio nao ndio hawa hawa.Tunaona machawa walivyopangwa kuwatetea eti tusiwaseme viongozi wetu!

Tunaona uwepo wa Mo ni kwa ajili ya kuifanya Simba iwe timu machachari kama KMC lakini ukweli haina malengo ya kwenda popote Africa.Usajili wa Chama ni dalili kuwa hawana mpango wa kuleta mbadala wa chama.

Simba itaendelea kuishi kwa kuchechemea na kupigania nafasi ya pili au ya tatu hadi viongozi kama mangungo waondoke,wafadhili kama mo aachane na Simba.Kama Singida na Ihefu wanapata wafadhili,itakuwa Simba?
Na sasa hata biashara United a.k.a wanajeshi wa mpakani wataanza kuwapangia nini cha kufanya hapo simba😅
 
Kuna wajinga wengi eti watakuamini kwamba umeandika points. Rudi darasani, fanya utafiti upya utagundua watu kama wewe ndo chanzo cha matatizo ya Simba. Badala ya kutafuta ufumbuzi sahihi wa tatizo mnatafuta Mbuzi wa kafara.
 
Back
Top Bottom