KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Wapinzani waliposhindwa kusimama mbele ya CCM na mwenyekiti wake katika uchaguzi wa Serikali za mitaa wanadai hakukuwa na uchaguzi ila uchafuzi na hii si mara ya kwanza kulalamika baada ya uchaguzi. Kususia uchaguzi na chama kupita bila kupingwa ni uchafuzi kwa mantiki yao. Tuachane na hayo kwa kuwa inawezekana kabisa mtu kupita bila kupingwa uchaguzi wa serikali za mitaa , na sababu ni: mtaani watu wanajua nani ana uwezo wa kushinda hivyo wengine wanaona hamna sababu ya kushindana na hii inakuja baada ya mtaa kuwa ni eneo dogo na lenye watu wachache.
Hapohapo CHADEMA wanasahau kujisitiri kuficha aibu kwa yatakayofanyika uchaguzi wa ndani wa chama chao. Haya mambo mawili yanatia doa uchaguzi wa chama chao na kuwa si uchaguzi ila ni uchafuzi mkubwa:
Mazingira hayo mawili yanaonesha nia, dhumuni na dhamira ya CHADEMA isivyo nzuri na katika kuweka kumbukumbu sawa, watu hawa watabadili katiba ya nchi ili mojawapo ya hayo mawili lifanyike. Wanaweza kubadili katiba ili waongoze maisha au wapite bila kupingwa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema ukizoea kula nyama ya mtu huwezi kuacha, hivyo ndivyo inavyoonesha kwa watani wetu hao. Uchaguzi wa 2020 tuwahoji hili swali ili mioyo yetu itulie.

- La kwanza, kuna uwezekano mkubwa sana Mbowe kurudi katika nafasi yake ya uenyekiti na kuvunja rekedi ya mwenyekiti aliyekaa muda mrefu zaidi madarakani baada ya Lipumba. Kwanini ni Mbowe wakati waliokaa madarakani muda mrefu wapo wengi? Kwanza, CHADEMA kimejimnanua kama chama kinachopigania demokrasia na moja ya hitaji la msingi la muhimu la kidemokrasia ni kuachiana madaraka na ukomo wa madaraka uwe unataka au hutaki. Je, CHADEMA chini ya Mbowe wametekeleza hilo? Ni demokrasia ipi wanayojivunia? Pili, Mbowe na wenzake ( CHADEMA) wanaeneza propaganda mbaya sana kuwa mwenyekiti wa CCM ni ‘dikteta uchwara’, je kukaa madarakani muda mrefu si kiashiria kimojawapo cha udikteta?
- La pili, kilichotokea kanda ya CHADEMA Pwani ndio kinasikitisha zaidi kuliko Mbowe kuongoza CHADEMA maisha. Ni aibu gani hii kwamba Kanda nzima ya Pwani ya kichama mtu akapita bila kupingwa. Wanashangaa mtu kwenye mtaa mmoja kupita bila kupingwa lakini hawashangai kanda nzima yenye mitaa zaidi ya 100 mtu kupita bila kupingwa.