Mwaka 2017 Kiongozi wa upinzani nchini Zambia (UPND) Hakainde Hichilema na wafuasi wake watano waliwahi kushitakiwa kwa makosa ya ugaidi kufuatia madai kuwa msafara wao ulizuia msafara wa rais Edgar Lungu, na hivyo kuyaweka maisha ya rais hatarini. Baadaye mastaka hayo yaligeuzwa kuwa ya Uhaini na Ugaidi na kutaka kuipindua serikali, lakini alikuja kuachiwa huru miezi minne baadae baada ya Jumuia ya Madola kuingilia kati.
Mashitaka kama hayo ndiyo yanayomkabili Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Freeman Mbowe anayeshitakiwa kwa tuhuma za ugaidi, ikumbukwe kuwa Hichilema na chama chake waliwahi kugombea urais mara 5 bila mafanikio kama ilivyo kwa chama cha upinzani nchini Chadema.