Kama MDDU Unit ya TANESCO ni Mali ya Maharage, Basi astaafishwe kwa manufaa ya Umma

Mkuu, ukisoma juu juu huwezi kuelewa. Ili uelewe hiyo Sentesi, elewa Nape Nnauye kwanini alisema Maharage kupelekwa TTCL ni Mshale kurudi nyumbani. Bado kapelekwa kwenye Wizara hiyo hiyo ya Nape Nnauye. (Nape, Makamba na Mwigulu ni Mapacha Watatu)

 
Makamba na huyu maharage wachunguzwe kuna mambo yamejificha hatuyajui. Yani makamba amfanyie vetting maharage hivi mama ulikua wapi wanakuingiza porini kiasi hiki? Huna vyombo au huvitumii?
 
Wa kulaumiwa hapa ni president mwenyewe. Ni muda mrefu sana watu wamekuwa wanapiga makelele kuhusu Makamba. Ila yeye aliamua kuweka pamba masikioni. Mpaka sasa yameshakuwa majanga ndo anajaribu kurepair. It’s too late. Makamba ni mwizi. Mwizi maarufu. Sijui bado anafanya nini kwenye ofisi za umma.
 
Wa kulaumiwa hapa ni president mwenyewe. Ni muda mrefu sana watu wamekuwa wanapiga makelele kuhusu Makamba. Ila yeye aliamua kuweka pamba masikioni. Mpaka sasa yameshakuwa majanga ndo anajaribu kurepair. It’s too late. Makamba ni mwizi. Mwizi maarufu. Sijui bado anafanya nini kwenye ofisi za umma.
 
Ahsante Kwa info classified.
 
Hivi kwanini mama abdul anaziba masikio kuhusu hili suala la kukosa uadilifu makamba na maharage?

Miaka miwili iliyopita walipokuwa wizara ya nishati wananchi waliopaza sauti zao sana na matokeo yamekuja kuonekana sasa baada ya Taifa kuingia gizani sasa anatapatapa kuwahamishia sehemu zingine wakaharibu tena

Inauma sana
 
Lakini mimi waziri wa nishati angeniletea hiyo bajeti ya mradi wa Trillion 11 , ningemuuliza kitu gani anaenda kufanya na tutapata Mega Wat (MG) ngapi ? maana kwa kutazama tu kwa haraka mradi wa Julius Nyerere ambao utazalisha MG 2100 utatumia Trillion 6, ningeshtuka tu.
 
DUNIA INA WATU WABAYA SANA, MABILIONI YOTE YA UIZI UTAZIKWA NAYO?, TUJIFUNZE KURIDHIKA KWA KIASI TUPATACHO, PIGA CHINI HAWA NA FILISI KABISA!
 
Ni kwa mujibu wa mkataba wa mwitongo ndio unaompa nguvu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…