Kama mlishangaa ya Kuchomwa moto Vifaranga Tanzania, sikia hii kali kuliko kutoka Uganda

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Juzi karibia Watu wengi tulipigwa na butwaa hasa pale ambapo tuliambiwa kuwa Vifaranga waliokamatwa wote wamepigwa moto tena bila huruma wala nini tukadhani haya mapungufu yapo tu huku Tanzania sasa leo Waganda nao wamejibu mapigo hali ambayo inaonyesha kuna uwezekano mkubwa Wasomi wengi wa siku hizi Afrika ya Mashariki wanavuta sana Bangi / Bange na zinawaharibu.

Ni kwamba Chama cha Madaktari nchini Uganda ( UMA ) kimepeleka ombi maalum kwa Kamati ya Bunge inayojishuhulisha na Sheria na Masuala ya Kibunge kuweza kuwaruhusu Madaktari wote wa nchini Uganda kufanya ' Utafiti ' wa Kisayansi wa kujua kama Binadamu aliyefikia Umri wa miaka 75 huwa ana kuwa na akili zake sawasawa au huwa zinamruka?

Ikumbukwe kwamba sasa hivi nchini Uganda kuna Kampeni ' maalum ' inafanywa na kuondolewa kwa kipengele katika Katiba ya nchi hiyo cha kuondoa ' ukomo ' wa Umri wa kuongoza Uganda ambapo inasemekana Rais Yoweri Kaguta Museveni ambaye muda wake ukimalizika atakuwa na miaka hiyo 75 hivyo bado anataka tena kuiongoza Uganda.

Mara baada ya Chama cha Madaktari wa Uganda kutoa hilo ombi ' Wasomi ' wengi wa nchini humo ' wamewacharukia ' Madaktari hao huku wakihoji kwamba imekuwaje ' Madaktari ' hao wameweza kukaa Vyuoni miaka 5 hadi 7 na kuweza kufanya ' tafiti ' zao mbalimbali za Kisayansi halafu wakasahau na kufanya ' utafiti ' wa umri na akili za Binadamu?

Na kilichowatia Waganda wengi ' hasira ' ni kitendo cha Viongozi wa Chama hicho cha Madaktari nchini Uganda kuitisha mkutano wao na Waandishi wa Habari wa nchini humo halafu wakati wanatangaza na kutoa hilo ombi lao karibia wote waliokuwepo meza kuu walikuwa wakicheka na kuonyesha ' Kejeli ' na ' Sanifu ' nyingi hali ambayo ilitafsiriwa kwamba walikuwa ' wanamdhihaki ' Rais wa sasa Mzee Yoweri Kaguta Museveni.

Kwa uhondo kamili wa mjadala huo mzito na malumbano ya Waganda tembelea mtandao wa Gazeti la Serikali ya Uganda la New Vision ujionee mwenyewe kila kitu ila hao ' Madaktari ' kitendo chao hiki kimewasha moto si wa kitoto baina ya ' Wasomi ' wa Kada mbalimbali wa nchini humo.

Am just thinking aloud kwamba hivi siku Chama cha Madaktari wa nchini Tanzania ( MAT ) nao wakiomba ruhusa kutoka katika ' Mamlaka ' ya Kibunge ya kufanya ' Utafiti ' wa kujua ni kwanini baadhi ya Binadamu huwa hawapendi na waoga kusafiri na Ndege au safari ndefu kwenda mikutanoni au kusalimia Marafiki zao itakuwaje au itapokelewaje.

Nawasilisha.
 
[emoji15]
 
naomna mtoa mada umeongea chunvi saaana na umeuficha ukweli wa hio story kamili
ombi la kupata maonibya madakitari lilitoka chama tawara na sio madakitari wariomba na kingine sio swala geni kwani mwaka 2015 dada wa kiiza besigye ambaye ni dakitari alichapicha kitabu kikiongelea hili swali na kikapigwa marufuku na serikari kuuzwa
wabongo bwana mwisho. yaani mtu yuko Tandale na anatoa story za uganda kama vile ako Kampala ambako tukio likitendeka
karibuni kampala mji usio lala ni biashara 24hrs
 
M7 mjanja sana hata ishu ya mashoga madaktari ndio waliobebeshwa bomu ili walipue yeye amalize mchezo. Madaktari walipewa kazi ya kufanya utafiti kama kweli binadamu anazaliwa akiwa shoga au anajifunza kutokana na mazingira? ndipo utafiti ukaonyesha ushoga ni kitu cha kujitakia akapiga marufuku. sasa anataka utafiti useme 75 anakuwa fiti ili aendeleze libeneke.
 
Back
Top Bottom