Kama mpira ni uchawi basi kamati ya usajili ya Simba isingepokea Matusi na lawama kwa kumsajili Sawadogo na Victor Akpan

Kama mpira ni uchawi basi kamati ya usajili ya Simba isingepokea Matusi na lawama kwa kumsajili Sawadogo na Victor Akpan

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kutokana na mashabiki wa Simba SC kukomaza mishipa ya Shingo na kutokwa povu la mdomo.

Kusema kuwa Yanga SC "inataka kutoa watu/viongozi/shabiki maarufu wa timu ndiyo ishinde mechi ya Algeria na ichukue kombe"

Hiyo kauli imenifanya nikumbuke mechi ya Simba vs Raja Casablanca ambapo Simba alichezea kichapo Cha tatu (3) kwa mtungi.

Kabla ya mechi makomandoo wa Simba waliweka guard /walikesha usiku kucha na wakichimba uwanja na kuweka vitu visivyo julikana.

Na wakati timu inaingia uwanjani tulishuhudia tukio la ajabu baada ya dereva kuingiza timu kinyume nyume lakini bado Raja Casablanca wakaichapa Simba bao tatu.

Kutokana na scenario hiyo inatufundisha mpira siyo uchawi /Imani zakishirikina Bali mpira ni kuwekeza/ kutengeneza benchi la ufundi imara na kusajili professional players.

Kila shabiki wa Simba SC mwenye akili timamu/asiyeamini uchawi hushinikiza viongozi wa Simba SC wasajili wachezaji wazuri ili walete makombe kwenye timu yao.

My take: Kama mpira ni uchawi/ushirikina Kama mnavyoamini hakuna haja ya kumtimua Sawadogo, okrah Akpan nk. Inawapaswa kuwaacha tu ili mtumie uchawi wenu huo mnao uamini kuchukua makombe.

Naitakia Kila la heri Yanga SC katika michuano ya fainali huko Algeria.
 
Ndio nilishangaa baadhi ya mashabiki wa Yanga kulalamika kuwa kufungwa kwao Taifa na USM Alger sio kiuwezo ila ni uchawi wa mvua ulioletwa na Simba.

Wakati kila mtu aliona kuwa uwezo wa wale jamaa ulikuwa mkubwa mno kulinganisha na wachezaji wa Yanga
 
Ndio nilishangaa baadhi ya mashabiki wa Yanga kulalamika kuwa kufungwa kwao Taifa na USM Alger sio kiuwezo ila ni uchawi wa mvua ulioletwa na Simba
Wakati kila mtu aliona kuwa uwezo wa wale jamaa ulikuwa mkubwa mno kulinganisha na wachezaji wa Yanga
Na mashabiki wa Simba wanasemaje??
 
Yanga mmeanza kuwewesekaa mapema yotee hii??
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na mashabiki wa Simba wanasemaje??
Mashabiki wa Simba wao wanaamini kilichowaua Yanga sio uchawi ni uwezo wao mdogo na pia Yanga haikuwa timu yenye hadhi ya kucheza Final hiyo imepelekea mechi ya fainali kuwa mechi nyepesi na ya upande mmoja kiasi cha USM Alger kuchukua kombe kwa kujipigia nyumbani na ugenini hii inaonyesha udhaifu wa wapinzani wake aliokutana nao Final
 
Kwa hiyo Simba ndiyo ilistahili kucheza fainali???

Na suala la kupigwa na Azam nalo mnasemaje Tena kwenye nusu muhimu kabisa ya kupata walau kombe la kufutia machozi.

Gwele
 
Back
Top Bottom