MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Leo nimesikitika sana baada ya kusoma uzi wa jamaa anayetaka wahudumu wa mgahawani kwa mshahara wa Tsh 2000/= kwa siku kwa hoja kwamba watakula bure mgahawani. Watu wengi kwenye ule uzi wamempinga vikali mleta mada. Mimi pia niliandika comments za kupinga huo ujinga.
Ninawasihi waajiri binafsi watoe ujira ambao mtu anaweza hata kulipa nauli ya daladala na kubakiwa hata na Tsh 2000/= kila siku badala ya huu utumwa wanaoutangaza. Kama biashara yako haina mzunguko mzuri ni bora ukakomaa kivyako na familia yako hadi pale utakapoweza kuajiri mtu mwingine. Au akijitokeza mtu wa kujitolea ndo umlipe hizo posho kuliko kusema eti ni nafasi za kazi wakati ni utumwa mtupu.
Hata wafanyabiashara wakubwa wenye viwanda wanatuhumiwa kulipa mishahara ya chini ya Tsh 5000/= huku watu wakipigika hatari. Utetezi wao ni kwamba wakipandisha mishahara watashindwa kuendesha viwanda. Huu ni uongo mtupu. Hao matajiri ni wabinafsi wasio na utu. Kama kwenye net profit kwa mwaka tajiri anaweza kujinunulia V8 la anasa au kujijengea hekalu anawezaje kusema gharama za ku-run ni kubwa? Pia kusema kodi ni tatizo ninapinga. TRA wanachukua kodi baada ya kuangalia gharama zako za uendeshaji. Ina maana kiasi kidogo utachoongeza kama posho kwa wafanyakazi kitajumuishwa kwenye matumizi ya kampuni na kupelekwa TRA.
Watanzania tupendane na tuache kukandamizana. Kama sisi wa chini tunakandamizana kamwe hatuwezi kuwa kitu kimoja na kukataa ukandamizaji wa baadhi ya viongozi.