Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Moja ya mambo yanayovuruga sana wanadamu ni mambo ya imani ambayo msingi wake ni kuamini bila kuhoji na kuhoji ni sawa na kukufuru(unamezeshwa).
Maajabu zaidi ni kuwa tuna vitabu viwili ambavyo ni Bibilia na Quran, lakini kwasababu watu wamekuja na tafsiri zao za haya maandiko, leo tuna madhehebu kibao kwa kila dini wakati Mungu tunaambiwa ni mmoja.
Matokeo ya hali nii mtu anazaliwa na kukulia katika dhehebu fulani mfano mkatoliki, baadae anahama anakuwa mlokole kwa hoja hawezi kukombolewa kupitia ukatoliki au mtu anzaliwa na kukulia katika ukristo, akikua anaona ukristo sio dini sahihi anahamia kwenye uislamu and vice versa.
Kituko kingine ni mtu kubadili dini kisa kuoa au kuolewa. Huu ndio uthibitisho hizi dini sometimes tunaburuzana tu na wala hatuziheshimu kabisa.
Sasa swali linakuja, kwanini mtoto anapozaliwa asiachwe mpaka awe mtu mzima awezi kufanya maamuzi sahihi afuate dini gani na dhehebu gani au asifuate dini kabisa?
Kama tunaona mtu mwenye umri wa chini ya miaka 18 hawezi kuwa na maamuzi sahihi kwenye sanduku la kura, ni kwanini kwenye mambo sensitive kama haya ya kiimani turuhusu watoto kuburuzwa na wazazi wao kiiamini kwa kutakiwa au kuachwa kufuata dini za wazazi wao?
Mtu anapobadili dini au dhehebu, huwa anatubu kuwa alikuwa amepotoka, na kama hatubu, hiyo dhambi ni nani anastahili kuibeba kama sio mzazi au mlezi?
Tukumbuke baadhi ya hizi dini na madhehebu yametokana tu na mitazamo/tafsiri za wanadamu kama sisi.
Tuwaache watoto mpaka watopofikia utu uzima(walau miaka 21) ndio wachague dini na dhehebu au kutokuwa na dini kabisa wakiona ni sahihi kufanya hivyo.
Tubadilike.