A
Anonymous
Guest
Habarini JamiiForums,
Nawaailisha kero yangu kwenu iwafikie Hospitali ya Muhimbili, wanachotufanyia tunaokuja kuona wagonjwa si uungwana.
Juzi July 10, 2024 nilikwenda kuona mgonjwa nikiwa nimeambatana na baadhi ya ndugu, kufika pale tukakatiliwa kuona wagonjwa tukiambiwa ndugu waliokwenda kuona wagonjwa wametosha, hii ni sawa?
Ndugu wanaingia wanne eti mnaambiwa hii imetosha wengine mje siku nyingine na walinzi wanawakataza kuingia, na hapo siyo kwamba muda umeisha!
Mtu umetoka mbali umepoteza nauli na muda wako kuja kuzuiliwa kumuona mgonjwa wako hii siyo sawa. Kama muda umebadilika watuambie, itatusaidia sisi kujipanga hata kwa kujiwekea zamu, lakini siyo unafika na unajua upo ndani ya muda unazuiliwa kwenda kumuona mgonjwa wako.
Sijapenda kabisa nilichofanyiwa juzi.