Kama Mungu ni muumba kwa nini aliumba binadamu mwenyewe tangu tofauti?

Kama Mungu ni muumba kwa nini aliumba binadamu mwenyewe tangu tofauti?

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,385
Reaction score
10,659
Katika dunia tupo binadamu wa rangi, nasaba, size na vino tofauti tofauti. Leo tujiulize moja tu, rangi zetu!
Ukiyachunguza mabara yote yanabinadamu wekundu, weupe na weusi ambao wapo weusi tii, rangi ya kunde au chocolate.

Katika rangi zote hapo juu ni rangi nyeusi inayoongoza kwa kudharauliwa, kuchukiwa na kufanyiwa mizaha. Binadamu weusi ni asili ya Africa japo hata huko India wapo black indies. Ni ajabu! Kila kitu chini ya ngozi tunafanana binadamu wote ila nje ya ngozi tu tofauti.

Watoto wachanga
Ni hakika, kila binadamu huzaliwa na nasaba za kizungu. Hakuna mtoto aliyezaliwa ni mweusi au mwekundu. Hali hii hupotea muda mfupi wakati wa ukuaji kwa waafrika.

Hakuna mweupe/mwekundu aliyeamua kutafuta dawa ya kujibadili awe mwafrika wakati waafrika baadhi kwa kudharau rangi nyeusi hujibabua kwa madawa au machine ili wawe weupe!

Kama Mungu yupo, kwa nini hakutuumba sote tuwe na rangi moja kuepuka ubaguzi?
Ni kitu gani huwabadili watoto wachanga wa kiafrika kuwa weusi? (Kama ni genes kwa nini wasizaliwe weusi?)
 
Back
Top Bottom