Kama Mwanayanga SC siwezi kumpigia kura Abbas Tarimba kwa nafasi yoyote TFF

Kama Mwanayanga SC siwezi kumpigia kura Abbas Tarimba kwa nafasi yoyote TFF

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
I declare Interest. Mimi ni Mwanayanga mpenzi wa mchezo wa Mpira wa Miguu.

Nmemsikia Tarimba Abas akiwa Bungeni na pia akihojiwa na vyombo vya habari. Ukimwona Bwana Tarimba kabla hajaongea unaweza sema atakuwa na Busara au Akili.

Akija kuongea utasikitika na kujiuliza kwa nini ameongea? Ni bora angenyamaza tumchukulie kuwa ana akili au busara kuliko kuongea na kutu prove tuliomfikira hivyo wrong.

Mimi kama Mwanayanga mwenye akili siwezi mpigia kuta Tarimba Abas wa nafasi yoyote pale TFF na hata inashangaza alipataje Ubunge.

Tuchagueni watu wenye akili kama akina Aly Mayai n.k but kama ikishindikana abaki Karia. Mimi sioni anachoipendelea Simba. Haya ni mawazo mfu kabisa. Mpira wa Simba inaonekana uwanjani. Wameenda mpaka Nafasi ya robo fainali Ligi ya Mabingwa leo unasema wanabebwa na TFF? hii akili ya wapi?

Simba imepoteza matches mbili kwenye ligi haikumlaumu mtu zaidi ya Wachezaji wake. Kipindi Yanga tunaongoza na hatujapoteza match hata moja. Tukianza poteana anatafutwa mtu wa kumwangushia jumba bovu.

La kusikitisha hata hawa watu tulidhani wangekuwa na akili kumbe nao ndo walewale. Alisema rafiki yangu mmoja "Hata Wapumbavu nao Huzeeka"
 
Angalau Wanayanga mmeanza kujielewa.

Wengi wanaosema Karia Hafai, wala hawasemi Hafai kwa sababu zipi. Na hata wakizisema utakuta ni shutuma zinazowahusu Bodi ya ligi.

Nakumbuka huyu Tarimba kipindi alipokuwa kiongozi wa Yanga aliwahi kuiamuru timu ya Yanga itoke uwanjani kwa kupinga maamuzi ya Refa.

Pia kuwa kwake kiongozi kwenye michezo ya Kubeti (Sportpesa) kunapingana na sheria za soka hivyo hafai kuongoza TFF.
 
Watu wa yanga bwana.. hata aje nani tff still team itakuwa ya hovyo sana kama wasipo change.

We angalia hata usajili wa wachezaji utaona utofauti, uendeshaji pia wa team

Wanataka aje nani pale tff ili amfanye sapong afunge magoli mengi[emoji3]

#mpira ni pesa, ukiwa na pesa hata wachezaj wazuri watavutiwa
 
Kwanza kajamaa kana TAMAA ya pesa sana pesa za wakamalia Sportpesa hazimtoshi??Ubunge nao pesa haitoshi?? Bado na Uraisi wa TFF? Khaa jamaa ni mroho wa madaraka na hana dhira ya Uongozi kabsaaa

Nasema uongo ndugu zangu?
 
Kama ni mwanayanga kweli basi wanayanga siku hizi mmeanza kujielewa.
Utopolo wenzio wanahisi Karia ndo anawafanya wasipate matokeo sijui huwa anakaa golinj anaudaka mpira uliopigwa na Sarpong goal machine[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Watu wa yanga bwana.. hata aje nani tff still team itakuwa ya hovyo sana kama wasipo change.

We angalia hata usajili wa wachezaji utaona utofauti, uendeshaji pia wa team

Wanataka aje nani pale tff ili amfanye sapong afunge magoli mengi[emoji3]

#mpira ni pesa, ukiwa na pesa hata wachezaj wazuri watavutiwa
Mapema wanaanza kuharibu rekodi ya mchezaji waliomsajili hawazioni sijui mechi 39 goli moja assist moja eti ligi ngumu what a rubbish wanafikilia hawa Kesho wanalalama karia nk

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom