Kama ni gaidi apelekwe gereza la Gwantanamo?

Kama ni gaidi apelekwe gereza la Gwantanamo?

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Wamarekani waliposhambuliwa na magaidi haraka haraka walitunga sharia kali za kupambana ugaidi na waliziingiza haraka katika sharia za kimataifa, haitoshi walimwaona gaidi kama kirusi cha hatari kuzidi cha Korona, fasta wakajenga gereza mbali sana nje ya nchi yao kule Cuba gereza la noma lijulikanalo kama Gwatanamo. Gaidi aliogopwa.

Gaidi hakutakiwa kutoka gerezani ila hakimu ndiyo alifunga safari kwenda Gwantanamo kusikiliza kesi ya mtuhumiwa, watu wanasema Marekani inaongoza kwa demokrasia lakini magaidi wa Gwantanamo hawakuwa wanapata msaada wa kisharia katika kesi zao. Hakuna waandishi wa habari walioruhusiwa kufika mahakamani, lakini mtuhumiwa gaidi hakuweza kuonana wala kuwasiliana na mtu yoyote hata mkewe.

Huku kwetu kwetu sielewi kwanini hatufanyi kama kila kitu tulivyo letewa na wazungu au kama tulivyopokeaga ukrisu ulivyoletwa au huyu si gaidi? au wanatudanganya. Gaidi kila siku anasafiriswa kwenda visutu. Gaidi anachupa za maji safi na leso ya kufuta jasho. Gaidi ni noma. Magaidi wa bongo tunakaa nao hata kama wametambulika wanakuwa mtaani badaade anakamatwa.
 
Wamarekani waliposhambuliwa na magaidi haraka haraka walitunga sharia kali za kupambana ugaidi na waliziingiza haraka katika sharia za kimataifa, haitoshi walimwaona gaidi kama kirusi cha hatari kuzidi cha Korona...
Mtoto wa mchunga kondoo,wakwetu ni magaidi wa kubambikiwa, ndio maana no marafiki viongozi na hata wafadhili wetu.
 
Back
Top Bottom