Kama ni kweli basi kazi IPO

Junior Clinton Mr.

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
1,075
Reaction score
1,423
Mnamo mwaka 2011 serikali ya Marekani kupitia raisi wake Barack Obama ilithibitisha kwamba May 2 ya mwaka huo kikosi maalumu cha maangamizo kilifanikiwa kumtoa kwenye uso wa dunia adui namba 1 wa Marekani, Osama Bin Laden.

Aliuwawa akiwa kwenye makazi yake Abboltabad, Pakistan kupitia oparesheni mkuki wa Neptune (Neptune spear) na mwili wake kuzamishwa baharini.
Daily mail waliandika kwenye kichwa cha habari "Kaoze kuzimu- Obama: Timu ya Wamarekani imemuua Osama kwenye pambano la moto"

May 2014, Snowden mpuliza filimbi, msaliti_shujaa anaibuka kwenye mahojiano ya siri na kituo cha Moscow Tribune na kusema "The famous terrorist and former leader of Al-Qaeda is ALIVE and receives benefits from central intelligence Agency, CIA"-- "Gaidi maarufu na kiongozi wa Al-Qaeda YU'HAI na anapokea fadhila kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA).

Anadai taarifa za kifo cha Osama zilighushiwa ili kumuongezea sifa na mvuto wa kisiasa raisi Obama kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2012. Snowden anaendelea "I have classified documents showing that Osama is still on CIA's payroll"-- "Nina document murua zinazoonesha kwamba Osama bado yupo kwenye malipo ya CIA".

"He still receives more than $100,000 a week which are being transferred through some front businesses and organisations directly to his Nassau bank account, I am not certain where he is now, but in 2013 he was living quietly in Bahamas in his Villa with his 5 wives and many children"-- "bado anapokea zaidi ya mil 209 tsh kwa week kutoka CIA, ambayo inahamishwa biashara na mashirika moja kwa moja kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau.

Sina uhakika alipo sasa, lakini mwaka 2013 alikuwa anaishi maisha ya kifahari sana Bahamas yeye na wake zake wa5 pamoja na watoto wake wengi"
Snowden alidai kwamba "Osama bin Laden ni mshirika (operative) mtiifu na makini wa CIA kwa muda mrefu sasa.

Je tukio la Marekani kumuua Osama lingefikisha ujumbe gani kwa washirika pandikizi wa CIA? Kwamba nao wajiandae kuuwawa? Anaendelea kudadavua kwamba Marekani ilipanga shambuluo la bandia la kumuua Osama kushirikiana na Pakistan Secret service na hili tukio limemkumbatia Osama na kumfanya awe salama zaidi, kwasababu kila mtu ameamini Osama ameuwawa, hivyo hakuna mtu atakayejishughulisha kumsaka.

Leo hii Snowden akiwa na makosa yenye kifungo cha jumla ya miaka 120 yupo mafichoni katika nchi za Urusi na Brazil. Baadi ya watu wanamuona kama Msaliti wa usalama wa taifa na baadhi ya watu wanamuona ni mwananchi mzalendo.
UKWELI UNAOTHIBITISHA KUWA OSAMA HAKUUWAWA KWENYE OPARESHENI GERAMINO.
☆Kivipi Osama afe mara mbili, ni lini alifufuka?

Wachambuzi wa maswala ya kijasusi, viongozi wa nchi, wakuu wa taasisi za usalama waliwahi kuzungumza kwamba Osama alifariki miaka mingi iliyopita (2001). Afisa veterani wa CIA Robert Beir, kiongozi wa zamani wa FBI kitengo cha kupambana na ugaidi (counter - terrorism, waziri mkuu wa zamani wa Pakistani Banazir Butto, Alex Jones wa CIA wote walidai Osama alifariki 2001. Katibu mkuu msaidizi wa Marekani Dr. Steve Pieczenik aliwahi kuthibitisha kwamba Osama alifariki kwa Marfan Syndrome na kwamba daktari wa CIA walifika kuupima mwili wa Osama akiwa hospitalini Dubai.


☆Mkanganyiko wa matukio ya oparesheni Geramino.
Kwanza tunaambiwa kulikuwa na majibizano ya risasi ya dakika 40, tena tunaambiwa hakukuwa na majibizano yoyote (kwamba mlinzi m1 wa Osama alitandikwa mkwaju akafariki na kisha kikosi cha FBI kikamfikia Osama.)
Tunaambiwa Osama alijeruhiwa vibaya, mara tena tunaambiwa Osama hakujeruhiwa bali alimtumia mkewe kama ngao.

Tunaambiwa makazi ya Osama yalikuwa ya ghali zaidi ya $1 million, ukweli ni kwamba kilikuwa ni kakibanda cha ovyo hata hakifiki robo ya huyo pesa.
Taarifa alizotoa Obama na maafisa wa usalama na intelijensia zilikuwa zinapishana sana.

☆Kutupa mwili wa Osama baharini.
Baada ya watu kushambulia kitendo hiko, Obama aliibuka na kusema kwamba walifanya hivyo kufuata utaratibu wa Ibada ya mazishi ya kiislam. Lkn wanazuoni wa kiislam wakapinga vikali hoja hiyo wakidai kwamba muislam anaweza tu kuzikwa baharini endapo alifia baharini.

☆Uchunguzi wa sayansi wa vinasaba na sura.
Viongozi wa usalama walidai kwamba vipimo ya DNA na uchunguzi wa sura (facial recognition) vilifanyika ili kuhakiki pasi shaka kuwa mwili ule ulikua ni wa Bin Laden. Je ni kwanini vithibitisho hivi havijawahi kuwekwa popote hadharani?

☆Kughushi picha ya chumba cha matukio (situation room).
Ikulu ilitoa picha ya ikulu ikimuonesha Obama, H. Clinton, Joe Bide na staff wengine wa ulinzi wakifuatilia shambulio lililomuuwa osama. Lakini baadae mkuu wa CIA, Leone Panette alikiri wazi kuwa Obama na team yake wasingeweza kushuhudia shambulio hilo 1 kwa 1 (live feed) kwani mitambo ya kurekodi tukio hilo ilizimwa ili isiingiliane na mawasiliano eneo la tukio.
Picha hii iliundwa mahsusi kumpa obama kiki ya kihistoria.

☆Tamko la Al-Qaeda.
Vyombo vya habari viliripoti kua Al-Qaeda wenyewe wamethibitisha kuuwawa kwa Osama. Lakini mchezo huu ulisukwa na shirika liitwalo SITE ambao ni mtandao maalumu wa kupika propaganda za shambulio la Pentagon. SITE ipo chini ya binti wa shushushu wa Israel mara kadhaa wamekuwa wakidakwa kutengeneza video kwa kutumia utaalamu wa juu kulingana na matakwa ya serikali.

☆Majirani wa mjengo wa Osama.
Majirani wa Osama ktk kijiji cha Abboltabad hawajawahi kuhisi tetesi zozote juu ya uwepo wa Osama hapo. Hata jeshi ya Pakistani ambalo lipo jirani walishindwa kung'amua uwepo wa Osama pia. Obama pia alithibitisha kua hawakuwa na uhakika 100% kuwa Osama alikuwa ndani ya lile jengo (ni kama kamari). Yawezekana waliuwa mtu tofauti kabisa na kuamua kuutangazia ulimwengua kuwa wamemuuwa osama ili kuficha aibu.

☆Osama alikuwa ni asset.
Asset katika dunia ya kiinteligensia ni kitu chochote chenye thamani/value ya kuweza kudukua taarifa muhimu. Gaidi aliyekamatwa porini ndiye aling'amua wapi Osama alipo, alikamatwa na kuhojiwa kwa mateso (torturing interrogation) ndipo akafunguka. Iweje Osama ambaye alikuwa gaidi most wanted na biggest asset asikamatwe ahojiwe ili kung'amua taarifa za ugaidi wa ulimwenguni. Moja kwa moja aliuwawa wakati lengo la Marekani lilikuwa kumkamata akiwa hai (kwanini walimuuwa wakati kulikuwa na uwezekana wa kumkamata akiwa hai).

☆Mbinu ovu za serikali ya Marekani.
Mara kadhaa serikali ya marekani imeshtukizwa kusuka mipango ya kijeshi ili kujiongezea sifa za kivita kimataifa mfano tukio la kumuokoa Jessica Lysch walipika mpango kufanya kama alitekwa na wanamgambo wa Iraqi na kisha jeshi la marekani likamwokoa (sawa na kujitekenya) pia hata kifo cha Pat Tillman yote ni mbinu za kughushi. Pia siku za usoni nitazungumzia moja ya matukio ya aina hii yaliyoidhalilisha marekani (oparesheni Misitu ya kaskazini).

☆Pia naandika uzi huu najiuliza je ni kweli Osama alikua na ulinzi dhaifu kiasi kile? Ni kwanini marekani walifanya shambulio hili bila kuwashirikisha viongozi wa usalama wa Pakistan.
HITIMISHO:
Obama, ikulu ya marekani, taasisi na mashirika ya ujasusi ya marekani na viongozi wa usalama wa Marekani hawajawahi kutoa tamko la kupinga/kukanusha filimbi aliyopuliza Bw. Snowden (Obama alijitahidi kujibu baadhi ya hoja za Snowden lkn suala la kifo cha Osama hajawahi kuligusa).
Niseme tu, taarifa za kuuwawa kwa Osama na kikosi maalumu cha Navy SEAL unit 6 ni jambo la kutiliwa wasiwasi na ni vizuri tujiulize kwa mapana zaidi.

Source: Social Network
 
Mambo ya wamarekani hutayaweza maana hata wewe unatafsiri ya kwao sasa Osama na Tz kunauhusiano? Walimtengeneza wao kwa maana hiyo wanaweza kuandika na kufanya watavyo
 
Sasa zile video zilizoonyeshwa namna wanavyoingia mle kwenye hekalu lake hadi wanamtaget zikukuwa niza uongo?na je.. mwaka juzi kama sijakosea wale sniper wawili walioshiriki lile tukio mbona walikuja kutofautiana kila mmoja akijitapa yeye ndio alianza kumshika ina maana ile nayo ikikuwa ni danganya toto?
 
Ukiweka mbali yote haya uliyoyasoma na kuyaanadika. Binafsi unaonaje, Osama yupo au alisjafariki kitambo?
 
Dunia hii ina mapicha picha mengi mno hata histpria ya tz nayo inasemakana ina mapicha picha cjui tuamini lipi
 
Kwa hiyo Osama yupo hadi Leo ila kama marekani ndo imemuhifadhi na inamlipa mshahara basi hakuwa adui yao maana kama wanamuhifadhi uwezo wa kumuua wanao pia na sidhani kama Trump baada ya kuingia madarakani akute wapinzani wake wamemtunza Osama na wanamlipa mshahara eti na yeye aendelee kumpa mshahara
 
Snowden...

Huyu jamaa anataarifa nyingi sana za mataifa mbali mbali... akiamua kuianika nchi fulani anaiacha uchi kabisa kwa uthibitisho wote...

Ni mtu mzuri sana kwa jamaa... ila anaonekana mbaya na hatari sana kwa serikali mbali mbali...


Cc: mahondaw
 
kweli aisee ukifikilia ni jambo lisilo wezekana
 
Huwa nikitizama September 11 nashindwa kumchambua bin laden ni pasua kichwa
 
Laden na Al Qaeda ni mpango wa USA kama ilivyo kwaIsis,Boko haram,Al shabab n.k
 
Osama amekuwa Trained na CIA agent anaitwa Mohamed Abdoul Saoul. Uwezekank ni kwamba na yeye alikuwa ni agent wa CIA.
 
Hii dunia ni ya kuacha hivi hivi maana mambo mengi ukweli wake ni mgumu kuupata.
 
Kuna mengi nyuma ya pazia!! Anayetambua siri za familia ni viongozi wa familia husika mengine mikwara!! Ila siyo mbaya kujifunza though kuupata ukweli bado saaaaana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…