Uchaguzi 2020 Kama ni kweli, Busara ya NEC, Vyombo vya Ulinzi, Viongozi wa Dini na wazee wa taifa hili iko wapi?

Uchaguzi 2020 Kama ni kweli, Busara ya NEC, Vyombo vya Ulinzi, Viongozi wa Dini na wazee wa taifa hili iko wapi?

Wamkopeka

Senior Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
136
Reaction score
308
Kama ni kweli haya tunayoyasikia katika mchakato huu wa uchaguzi, kuenguliwa kwa idadi kubwa ya wapinzani kwa kile kinachoitwa kukosa sifa. Je, wahusika hawaoni kuwa hii hali inaweza kupelekea vurugu zisizokuwa za lazima?

Hivi inakuwaje hiyo kukosa sifa kunatokea upande wa wapinzani tu? Je, ni sifa gani hizo ambazo wapinzani wamazikosa kwa idadi kibwa namna hiyo na hakuna hata mgombea mmoja wa CCM aliyekosa hizo sifa?

Je, Nec, Vyombo vyetu vya Ulinzi, Viongozi wa Dini na wazee wetu wastaafu, mnakubaliana na mwenendo huu? Siombei itokee lakini najiuliza tu ikiwa upizani utakosa uvumilivu katika hili na kama ambavyo tumesikia matamko yao mbali mbali, Je mtajiweka katika nafasi gani?

Kwa miaka mingi nchi yetu imejizolea sifa kuwa kisiwa cha Amani, na wengine tuliobahatika kufika nchi za watu tulekuwa tukitamba kuwa tunatoka kwenye kisiwa cha Amani.

Sasa ni vema tukaendelea kuidumisha hiyo sifa kwa kuzuia viashiria vyote vinavyoweza kuharibu amani yetu.

Binafsi natamani kuona Nec wanarekebisha hii hali mapema iwezekenavyo. Na kama kuna ulazima wa kumuengua mtu basi iwe ni kwa sababu zenye mashiko, (1) kama kutokuwa raia wa tanzania kwa kukosa vigezo vyote vya uraia sio kusingizia.(2) kuwa na mashitaka ya kutenda jinai.(3) kukosa maadili tena kwz ushahidi usiokuwa na shaka.

Katika hili haki itendeke, haileti picha nzuri kwamba wanaokosa sifa ni upande wa upinzani tu. Tuipende nchi yetu na tuilinde kwa kuanzia na kupendana sisi kwa sisi bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini, maumbile yetu, makabila yetu, rangi zetu, au eneo tunalotoka na tuamini kwamba yeyote anayechaguliwa anaenda kufanya kazi ya kuiletea maendeleo Tanzania yetu.

Tuwaache wagombea watoe sera zao na Watanzania wapiga kura wawe ndio waamuzi wa mwisho. Sisi sote ni Watanzania tutendeane kama Watanzania.
 
Kamati ya amani inaongozwa na Sheikh Alhad Musa.

Ana Prado mpyaaa.
 
Na mbaya zaidi CCM ina wagombea mpaka wenye elimu ya std 7 lakini hawajakosea... So sad
 
Kamati ya amani inaongozwa na Sheikh Alhad Musa.

Ana Prado mpyaaa.
Unawaongelea akina shekhe Mussa Salum? Unaongelea akina Gwajiboy? Akina Mtokambali? Hao sio viongozi wa dini, hao ni viongozi wa vibahasha, nchi hii viongozi wa kiroho ni wachache sana
 
Ni mambo ya hovyo ccm wanaharibu umoja wa taifa letu kwa maelekezo haramu.
 
Umepewa hela ya kujenga msikiti na mgombea urais, unaweza ukataka kuona anakuwepo wa kupambana naye kwenye uchaguzi?
 
Ni ubaya uliyozidi kipimo. Ajabu si viongozi wa dini wala vyombo vya usalama vyenye kuangalia mustakabali wa Taifa letu ambapo tunazungumzia raia jinsi linavyokwenda. Na wanaoleta mapenzi ya chama kuliko ya utu yenye kujenga Taifa sishangai. Nilichogundua ni kuwa kama mtu hana uzuri ndani ya moyo wake hawezi kuuona wala kuutambua uzuri wa nje anaouona kwa macho yake.

Kwa sababu kila kitu kinaanzia na kutokea ndani ya moyo, msukumo nje ya mwili kuyaendea ni matokeo yake. Kama mizizi ya moyo ikajikita kukithiri kwenye uovu mtu wa namna hii hawezi kuuona kuutambua uovu wa nje anaouona kwa macho yake. Mtu wa namna hii ni muovu.

Muda mwengine yanakuwa ni mapenzi, mapenzi yakiteka moyo wa mtu mhusika anakuwa haambiliki anaangukia kwenye uhayawani wa mapenzi. Athari zake zinaonekana pia! Jamii imeshuhudia miongoni mwa watu kufanya lolote imma liwe la shari au la heri ili kulienzi penzi, wengine hufikia pabaya hujitoa mpaka uhai. Mithili ya mapenzi ya namna hii ipo kwenye uvyama pia.

Ijapokuwa mhusika kwa namna moja ama nyengine naye anaangukia kwenye kundi la waathirika wa utawala usiyo na haki na huruma lakini mapenzi ya uchama yamemtia upofu wala hayaoni hayo. Mapenzi ya uhayawani ni majanga makubwa kwani kinachofanya kazi ni hisiya na si akili. Mwenye mfano wa namna hii ni mtu mwenye kutia hasara kubwa.

Vyombo vya ulinzi na usalama vina dhima kubwa sana. Mambo yanayofanyika kwa sasa yanavunja umoja wa utaifa. Na hapo ndipo usaliti wa nchi unapozaliwa na raia. Kurubuniwa inakuwa ni rahisi sana. Ila akili ya Mwafrika haipimi athari ya kitu kwa kukitafakari au kwa historia wao watasema Tanzania bado kabisa mambo kama hayo hayawezi kutokea tutayadhibiti. Akili ya Mwafrika inajua huu ni msala baada ya msala kutokea. Vyombo vya ulinzi na usalama vimejawa ulimbukeni wa hali ya juu.

Viongozi wa dini wanachukua nafasi kubwa kwenye jamii. Hususani jamii yetu. Sikia! Ikiwa kiongozi wa dini mwenendo wake ni kulitafuta sikio na macho ya mtawala, kiongozi wa dini wnamna hiyo atahudhurisha elimu yake ya kidini kwa kumsifia mtawala kwa matumaini huruma ya mtawala itamshukia eidha kwenye mambo yake ama kuruzukiwa zawadi mbalimbali au kupewa nyadhifa za kitaifa.

Viongozi wa dini wa namna hii wataitoa elimu yao ya dini kwa lengo la kumnufaisha mtawala. Watakuwa na uoga kwa mtawala na watakuwa wamejisalimisha kwenye mikono iliyodhibitiwa na mtawala. Muelekeo wao itakuwa ni ile ramani ambayo mtawala atakayowachorea. Kiongozi wa dini wa namna hii ni muovu. Sikia! Ikiwa kiongozi wa dini ataishi kwa kile alichojifunza kwenye miongozo ya dini ambayo ina sisitiza haki. Akawa anaishi kwa hayo kwa vitendo na kauli, na kwa hakika huu ndiyo uhalisiya wao! Hawawezi kuishi kinyume na hivi! Ni kama samaki ndani ya bahari, hawezi kuishi pasipo na maji.

Kiongozi wa dini wa namna hii amejisalimisha na kujielekeza kwenye njia ya Mungu. Wanakuwa webarikiwa na wanakuwa kwenye malezi ya uongofu wa Mtume(Mitume na Manabii). Kwa kila ambaye atakayeishi kwa zama zao ataguswa na wao. Viongozi wa dini wa namna hii wanakuwa wapo huru kutoka kwa watawala. Wanakuwa ni kama Jua, kazi yao ni kuangaza tu pasipo lenyewe kufaidika kwa kile linachotoa. Wanakuwa wamesoma kwa ajili ya kutoa, si kusoma kwa ajili ya kupokea. Huyu ndiye kiongozi wa dini anayetufaa.

Muda ni mwalimu mzuri! Heri na shari zitakazotokea zitatujuza msimamo upi ulikuwa ni sahihi. Athari inatungoja pia.
 
Back
Top Bottom