Kama ni kweli stendi ya Simu 2000 kubadilishwa matumizi na kuwa karakana ya DART ni kuwakosea wana Ubungo

SE-CHANDO

Member
Joined
Oct 18, 2023
Posts
5
Reaction score
2
Hizi habari za kusikitisha na kuumiza sana kwa wakazi Ubungo,

Nilivyosikia ni kuwa Stand ya Simu2000 inataka kubadilishwa matumizi na kuwa KARAKANA YA DART,
Kama habari hii ni yaukweli basi niswala lakusikitisha na kuwakosea wanaubungo.

Kubadilisha Matumizi ya stand hii na Soko ni muendelezo wa uporaji na unyanyasaji wa wananchi wanyonge ambao wanatafuta chochote kitu kutokana na uwepo wa stand hiyo na soko pia.

Nikiangalia kwa mapana zaidi naenda kuona eneo hilo likielekea kufa kiuchumi na hata wakazi na wananchi wa hapo wanaeleka kufa kiuchumi.

Nachoshangaa nikuwa eneo hilo lina mbunge ambaye ni waziri, mkuu wa wilaya ambaye ni kijana na diwani ambaye nikijana pia hivi unaachaje wananchi wako wa pale takribani elfu 10 wanaenda kufa kiuchumi na nyinyi mpo tu katika eneo hilo. Pia Halmashauri inaenda kupoteza chanzo muhimu cha mapato

Nilivyosikia nikuwa karibia Milioni 600 hukusanywa kila mwaka katika eneo hilo, Hizi pesa zinazokusanywa tu hapa, kwenye halmashauri zingine ndio pato la ndani la halmashauri yote kwa mwaka mzima.

Kuifanya eneo hilo kuwa Karakana nikuwakosea wafanyabiashara elfu 3 waliopo eneo hilo kuwakosea wakazi wa Ubungo na kuwakosea watumiaji wa stand hiyo takribani elfu 40 wanaopita na kufanya matumizi ya hiyo stand.

Niwakumbushe tu 2025 siyo mbali na mnamuonea Mh Rais kwa kumsingizia kuwa kila agizo linatoka kwake, tunapata shida sana sisi kama wadau kuendelea kuzungumzia mazuri ya Mh Raisi wakati kunawatendaji wake ambao wanaharibu kila kukicha.

Mdau wa Maendeleo Tanzania
Se-chando
 
Kama ni kweli basi kutakuwa na shida mahali. Karakana ya UDART ni ile iliyokuwa stand ya mkoa ya zamani ambayo sasa hivi wamepewa wachina wajenge soko lao na linakaribia kwisha. Naomba niishie hapa hapa.
 
Nadhani wameona walichoweka pale ni uchafu unachafaua taswira ya ile complex.

Ila muhimu nikuwa kwanini wasiende maeneo ya kibaha huko mwisho wa ruti yao watake mjini tu?
 
Ni lazima iyo stendi iwe ili stendi mpya ya mwenge ipate uchangamfu na route nyingi nyingi. Hofu yangu kwenye ufunguzi wa stend ya mwenge kutazidi kuongeza msongamano mwenge.

Mfano gari za mbagala, segerea, tabata zilizokua zinaishis simu 2000 sasa zitashusha mawasiliano zitaendelea hadi mwenge.

Changamoto ni gari za boko na bunju haziwezi ishia mwenge kwa abiria wa ubungo nafikiri zitakua zinageuzia mataa ya ubungo. Ila ngoja tuone
 
UDART wanunue eneo walipe watu wasitake kila kitu kutafuniwa maana hawana ushindani wa kugombania abiria ila naona wapo hovyo hovyo tu.
Pale ubungo bus terminal zamani
Ndiyo ilitakiwa kuwakarakana yao
Naona sahv pale kapewa mchina
Hivi ile karakana yao kule kurasini ipo
Bado

Ova
 
Usafiri wa Mabasi Yaendayo haraka kwa Wananchi wote ni muhimu

Ni kweli kuwa kuna Karakana itakayojengwa katika eneo la Simu2000 na Karakana hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa BRT awamu ya nne, inayoanzia katikati ya JIJI kwenda hadi Tegeta DAWASA, ikijumuisha barabara za Bibi Titi, Alihassan Mwinyini, na Bagamoyo, pia ina tawi linaloanzia Mwange hadi Ubungo eneo la Simu2000 kupitia barabara ya Sam Nujoma, ikiwa na jumla ya kilomita 30.1.

Karakana hii ni muendelezo wa mradi wa Mabasi yaendayo haraka kama mnavyoona kwa sasa mpaka Mbangala miundombinu imekwishajengwa hivyo Serikali haitaki kuona mwamanchi anapata adha ya usafiri kila eneo linafikiwa kupitia mabasi haya yaendayo haraka (Mwendokasi).

Ile Karakana ya Ubungo ni kwa ajili ya BRT 1 ndio inasarve pale lakini kwa hii ya awamu ya IV ndio Karakana yake itakua Pale Simu2000.

Mradi huu wa amwamu ya nne ukikamilika utakuwa na Mabasi yapatayo 590 yanayotarajiwa kusafirisha abiria wasiopungua 900,000 kwa siku.

Aidha, mbali na ujenzi wa Barabara za Mabasi, mradi wa awamu ya nne, utajenga vituo vya Mabasi 39, vituo vikuu (terminal) 3, upanuzi wa madaraja ya Salender, Mlalakuwa, Kawe na Tengeta. Pamoja na ujenzi wa Karakana (Depot) mbili moja Eneo la Simu2000 na nyingine eneo la Mbuyuni.

Lengo sio kuwaumiza wananchi leo ni kupata maendeleo ya pamoja na kwa sasa Manispaa ya Ubungo inaendelea na mipango ya kuwaweka mazingira bora wafanyabiashara hao watakaohamishwa katika eneo hilo.

Taarifa sahihi ni kuwa wafanyabiashara waliopo pale hawazidi 150 na wataandaliwa utaratibu mzuri wa kuendelea kufanya biashara zao ili huduma za usafiri wa mabasi yaendayo haraka ziweze kufikishwa kwa wananchi wa maeneo ya Tegeta nk

Nia ni Njema wala hakuna atakayeonewa.

Sent from my Infinix X6716B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom