MKWEAMINAZI
JF-Expert Member
- May 28, 2023
- 930
- 1,304
Cheo cha Naibu Waziri kuu hakipo kwenye katiba iliyopo lakini Marais waliotangulia waliwahi kumteua hayati Mrema na Salim Ahmed Salim kukitumikia cheo hicho.
Jana Rais Samia kamteua Doto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hakipo kwenye Katiba. Najiuliza kama cheo hiki cha Unaibu Waziri Mkuu kina tija kiutendaji kwanini hakiingizwi kwenye katiba?
Nauliza hivyo kwa sababu hata mafao ya cheo hicho hayajulikani na mwisho wa siku mhusika baada ya kukitumikia cheo hicho anapodai mafao yake huyakosa na huambiwa aonyeshe wapi katiba inayataja. Mfano mzuri ni hayati Augustino Mrema aliyadai bila mafanikio.