Mkuu Mestod, Kwanza pole sana kwa masaibu mazito yaliyokufika. Japokuwa haijanitokea lakini ninaamini inaumiza sana. M'mungu akupe nguvu na kukuongoza bro. Pili naomba nitofautiane na wale waliosema kuwa ni ndefu, kwa kweli mi sioni kama ndefu sana, kwani inatumia muda gani kuisoma jamani??!!! Yaani leo ndiyo nimeamini kuwa watanzania ni wavivu sana wa kusoma. Yaani watu wanataka sredi yenye mistari miwili au mitatu.........inasikitisha sana.
Wito: Tujitahidi kuwazoesha hata watoto wetu tu tabia ya kupenda kusoma maana inaonekana sisi wenyewe imetushinda.