Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KAMA NINGEKUWA ADUI YAKO, UNAFIKIRI NINGEANZA KUKUCHUNGUZIA WAPI?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Unapoingia katika uadui na mtu yeyote. Hapana shaka huwezi kufanya shambulizi lolote bila kumjua adui yako. Lazima ujue unapambana na mtu wa aina gani. Na hapo ndipo suala la ujasusi, upelelezi, uchunguzi linapoingia.
Ilimradi unaishi, huwezi kukosa maadui. Ilimradi unamaadui huwezi kupuuzia suala la elimu ya ujasusi.
Mtu kabla hajamchukua mkeo/mumeo lazima akufanyie upelelezi.
Mtu kabla hajakusagia kunguni kazini, ofisini kwa boss wako lazima akuchunguze apate taarifa zako.
Mtu kabla hajakuloga na kukuwangia lazima upelelezi ufanyike.
Kabla hujaangushwa kibiashara au kutolewa kwenye laini na washindani wako kibiashara lazima wakuchekeche, wakusomee ramani, wakuchunguze.
Sasa leo Mtibeli nitajigeuza adui yako wa siri au kificho. Then nitakuambia nikiwa kama adui yako nitaanzia wapi kupata taarifa ili nikujue kabla sijakupiga kata funua matata.
Niite TaikonMaster, mtibeli Adui kuu anayetaka kukupiga kata funua.
Hebu tufanye jaribio la akili.
Lakini Usikasirike wala Usiniogope. Usichukulie hii kama tishio. Sio nia yangu hiyo. Ni thought experiment tu.
Kama ningekuwa adui yako, ningekuchunguza wapi?
Je ningeanza na nyumba yako?
Au kukupora simu yako?
Au akaunti zako za benk na pesa zako?
Niambie. Unafikiri ningeanzia wapi?
Nichukulie kama Adui yako wa Heshima.
Ningeanza na tabia zako.
Kwa sababu mtu anayejua tabia zako anaweza kukisia hatua zako kabla hujachukua hatua. Yaani kujua next moves zako.
Mambo ambayo ningechunguza kuhusu Tabia zako. Na faili lako Zima lingekuwa mikononi mwangu;
1. NINGECHUNGUZA KITU UNACHOKIPENDA SANA
Kwenye kitabu changu cha The Chess Game; Niliandika mtu hutawaliwa kupitia mambo haya makuu matatu. Moja, kile anachokitamani na kukipenda(upendo na tamaa),
Pili, kile anachokiogopa(Hofu)
Tatu na mwisho, Kile anachokitumainia (Imani).
Kwa sababu kile unachokipenda sana kinaweza kuwa sehemu ya udhaifu wako.
Mtu anayependa pesa sana anaweza kushawishika kwa pesa.
Mtu anayependa sifa anaweza kudhibitiwa kwa sifa.
Mtu anayehitaji sana kupendwa anaweza kudanganywa kupitia mapenzi.
Mtu anayehitaji kuheshimiwa anaweza kuchokozwa kupitia heshima yake.
Kila tamaa ni mlango wa watu kukudhibiti, kuingia katika maisha yako.
Mtu mwenye akili haanzi kutafuta mahali unapoishi. Huangalia kile unachokipenda na kukitamani. Kwa sababu huo ndio mlango wa Akili yako ulipo.
Anaanza kutafuta mlango wa akili yako.
2. NINGEANGALIA KITU KINACHOKUKASIRISHA
Hasira kimedani ni chanzo kikuu cha taarifa. Kwamba mtu akitaka kukujua moja ya mambo ataangalia ni mambo yanayokukasirisha. Usiyo yapenda. Ni kinyume na kanuni ya kwanza.
Kwa sababu mtu mwenye hasira anaweza kujifunza kujificha. Lakini ni vigumu kuficha kile kinachomkasirisha kila wakati.
Hapa nitaangalia;
Ni nani anayekukasirisha?
Ni maneno gani yanakufanya ubadilike?
Ni aina gani ya dharau huwezi kuivumilia?
Ni jambo gani likiguswa, akili yako huacha kufanya kazi kwa utulivu?
Kila jibu la maswali hayo ni taarifa muhimu kumhusu mhusika
Mtu anayekujua vizuri anaweza kutumia hasira yako kama ramani ya vita kukuangusha.
3. NINGEANGALIA UNACHOFANYA UNAPOKATALIWA.
Tunaangalia rejection. Katika rejection law. Kuna kanuni muhimu ambazo adui huzitumia kupata taarifa zako.
Kwa sababu watu wengi huonekana werevu wakati mambo yanaenda vizuri. Wanapokubaliwa.
Lakini tabia halisi hujitokeza mtu anaponyimwa anachotaka.
Katika siasa, watawala huweza kukujaribu kwa kukupiga pin, kukukatalia jambo lako kimakusudi ili wakujue wewe ni nani. Na kama hujui kanuni hii unaweza kujikuta umekwama.
Unaponyimwa kazi, unafanya nini?
Unapokataliwa na mwanamke au mwanaume unayemtaka? Unamjibuje?
Unapopoteza pesa au biashara kwenda kombo? Unachukua uamuzi gani?
Unapodhalilishwa iwe mtaani au mitandaoni unafanya nini?
Unapopuuzwa unachukua hatua gani?
Reactions zako ni taarifa muhimu kukutambulisha wewe kwa watu na adui zako.
Je, unatafakari?
Au unalipiza kisasi?
Je, unaondoka kimya?
Au unaanza kutangaza siri za mtu?
Hapo ningejua kiwango cha udhibiti ulio nacho juu ya nafsi yako. Kujidhibiti ni kudhibiti wengine. Unaposhindwa kujidhibiti unafungua mlango wa kudhibitiwa
4. NINGEANGALIA MARAFIKI ZAKO
Binadamu ni kiumbe kinachoweza kujificha sio kwenye kichaka tuu bali kuficha utambulisho na tabia zake. Hii ni tofauti na wanyama wengine ambao wao huweza kujificha kwenye vichaka na mashimo lakini hawawezi kuficha tabia zao.
Kwa maana hiyo sisi Watibeli kwa kulijua hilo. Wakati mtu anahangaika kujificha sisi tunaangalia watu wake wa karibu. Rafiki zake.
Watu anaowachagua wanaweza kumfunua. Kwa sababu mtu anauwezo wa kujificha kwa tabia yake lakini hawezi kujificha kwa tabia ya mtu mwingine.
Katika Mahakama kanuni hiyo ni muhimu na inazingatiwa. Hata katika kanuni za ushahidi.
Ningeangalia;
Unatembea na nani?
Unawaheshimu watu wa aina gani?
Ni watu gani unaowaita “marafiki” hata kama wanakuharibu?
Unapokuwa na shida, unampigia nani simu?
Kwa sababu mara nyingi mtu hujengwa na watu anaowaruhusu kuwa karibu naye.
Na mtu humwamini mtu anayefanana naye kwa kiwango kikubwa.
Na kama ningekuwa adui yako, ningejua kwamba kumuelewa rafiki yako wa karibu kunaweza kunipa picha fulani kuhusu wewe.
5. NINGEANGALIA RATIBA YAKO
Mwanadamu ni kiumbe wa patterns na codes
Ningejiuliza;
Unaamka muda gani.
Unaenda wapi mara kwa mara.
Unafanya nini ukiwa na stress.
Ni siku gani huwa unakuwa busy.
Ni wakati gani huwa unakuwa peke yako.
Ni wakati gani unakuwa social.
Mambo haya yakikusanywa kwa muda yanaweza kutoa picha ya maisha ya mtu bila yeye kutoa siri zake.
6. NINGEANGALIA UDHAIFU WAKO WA KIHISIA
Kila mtu ana sehemu ambayo akiguswa, anabadilika. Ingawaje mwanadamu habadiliki. Nazungumzia reactions zake zinamtambulisha alivyo.
Ningeangalia je udhaifu wako upo kwenye nini?
Je ni familia, ni pesa, ni mapenz, ni heshima, ni watoto, ni hofu ya kuonekana amefeli.
7. NINGEANGALIA UNACHOJISIFIA NACHO
Hasa kile unachotamba nacho mara kwa mara.
Hili ni jambo ambalo watu wengi hawalijui.
Mtu anapojisifia sana kuhusu jambo fulani, wakati mwingine anakuwa ametoa taarifa kuhusu kile anachotaka wengine wakione kwake.
Mtu anayesema kila mara:
Mimi ni mwanaume wa heshima.
Mimi ni mwaminifu sana.
Mimi sihitaji mtu nataka niwe single.
Mimi nina pesa.
Mimi nina connections.
Usikimbilie kumwamini. Usilibebe kama lilivyo. Sikiliza anachosisitiza.
Kwa sababu wakati mwingine mtu anapojenga picha yake kwa nguvu sana, anakuonyesha picha anayohofia wengine wasiiweke juu yake. Unaelewa?
Kama hujaelewa, mara nyingi mtu hujisifia kitu ambacho anatamani kingekuwa kweli. Ni matamanio.
Adui makini akishajua hilo unajua atafanyaje? Hilo ni somo la siku nyingine
8. NINGEANGALIA KITU UNACHOKIFANYA MARA KWA MARA
Hii ni ichukue hata wewe. Itakusaidia sana.
Ukiomba msamaha mara kwa mara baada ya kukosea, kuna pattern.
Ukianza miradi mingi na kuiacha njiani, kuna pattern.
Ukiingia kwenye mahusiano na watu wa aina ileile na kila mara mwisho ni uleule, kuna pattern.
Ukiwa na ugomvi na kila mtu, kuna pattern.
Pattern ni tabia inayojirudia mpaka inakuwa taarifa.
Na mtu anayejua kusoma patterns anaweza kukuelewa bila wewe kumweleza maisha yako yote.
Sasa umeshajua ningekuwa adui yako ningeanzia wapi kukuchunguza. Jiulize ningeanzia wapi kukushambulia?
Wakati unatafakari.
Nimeandika post hii ili msomaji ujifunze namna ya kudhibiti taarifa zako. Uwe na self control. Ujidhibiti. Hii itakusaidia sana sehemu nyingi sana. Na adui zako hawatakushinda kirahisi.
Acha nipumzike sasa
TaikonMaster
Kwa sasa Kahama, Shinyanga.