Kama ningeyajua haya nisingeitoa mimba yangu ya karibu miezi minne

ukishaingia chama cha walioolewa ndipo utajua kama mada yako ni sahihi au la!
 
biology ya o level tu ilimtosha kujua kuwa alitoa mimba ya binadamu na si mdudu,hakujua lipi hapo?!
 
duh!huwa naumia sana nikisikia mtu ametoa mimba. ila kujuta kwake ni dalili nzuri hata muumba pia atamsamehe akitubu. mimi naamini kuanzia ile siku ya kutungwa mimba tayari ni uhai so whether utoe ya two weks au 4 months bado umeharibu uumbaji uliokuwa na kusudi maalum katika hii dunia. natamani ningeweza kumsihi kila msichana asitoe mimba. angalau tumwogope MUNGU jamani. ukishatenda kosa basi kubali matoke.
 
ukishaingia chama cha walioolewa ndipo utajua kama mada yako ni sahihi au la!

Unajuaje Kama sijaolewa.
Kwa hiyo ndoa ni excuse ya kuuA watoto?wee ukiuliwa kwa sababu yeyote ile utaona wauaji wako ni wakAtili?au kwa vile kichanga hakiwezi kujitetea?
 

Ni kweli kabisa mkuu.bora wanaojuta kuliko wanaofanya na hawajutii na zaid wanatumia nguvu nyingi kutetea hicho kitu.
 

queenkami,hapa ndipo nilipojua status yako,anyway na mimi nilikuwa na msimamo kama wako kabla ya ndoa kuhusiana na utoaji mimba.ila sasa huo msimamo sina kabisa!na usidhani kwamba kuna anyependa kufanya hivyo,bahati mbaya zipi,tena zipo nyingi sana,sio kwa rafiki yako tu hata wanawake wengine,na wala usidhani kwamba watu hawatumii kinga za kuzuia mimba,kwenye ndoa kinga unatumia lakini bahati mbaya za mimba kuingia zipo.samahani kama nimekukwaza!
 

Mkuu hujanikwaza ila na Mimi naomba nisikukwaze kwa kusema kuwa kwa kweli bado msimamo wangu ni ule ule.
 
Wakuu Nina Swali,hivi inawezekana vipi kutofautisha uhai na binadamu ?Kinachofanya binadamu awe living organism si ni uhai?hivi binadamu anaweza kuwa binadamu bila kuwa na uhai?uhai unapoondoka ktk mwili wa binadamu si jina Linabadililka na kuwa Maiti ya binadamu ?iweje mtu aseme mimba Eti mimba ikiwa Changa ni Uhai lakini sio binadamu?uhai ni nin na binadamu ni nin?
 
 
Maty hakuna comment humu itaweza badil msimamo wangu.narudia tena bora nife kuliko kunywa maji ya mwanamke muuaji,kwangu Mimi mtoa mimba Hana tofauti na Hitler tofauti Yao ni idadi ya binadamu waliotoa roho zao.mwanangu akiamua kutoa mimba hiyo ni laana Yake hainihusu ilimradi Mimi sikumuua yeye.wanawake wanaotoa mimba ni makatili sana,Kama wanaweza kuuA watoto waliobeba tumboni Kwao sidhani Kama wanashindwa kuwapa sumu waume zao au ndugu zao au hAta rafiki zao.once a killer always a killer.
 
queenkami, kama mimi sitaki ubadili msimamo wako wa kwamba watoaji mimba ni wauaji kwani huo ndio ukweli, ila kusema unamtenga hata akikupa maji huwezi kunywa hauko sahihi, ndio maana nimekuuliza ikitokea binti yako ametoa mimba utamkana kama unavyokana hapa? yaani ndio itakua mwisho wa yeye kukuita mama kwa sababu ni muuaji?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…