Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Mara nyingi nimesema kwamba Polisi Tanzania wanafanya kazi kwa namna ambayo ni very unprofessional na kwa lengo la kuwafurahisha CCM. Wanajikomba, wanajipendekeza kwa CCM kupita kiasi, hadi inatia aibu na kichefuchefu.
Sasa katika tukio la Mbeya la viongozi wa Chadema kukamatwa, Dr. Nchimbi ametoa agizo kinamna kwamba Polisi wawaachie viongozi wa Chadema waliowakamata. Sasa kama Polisi walikuwa na sababu za msingi kuwakamata viongozi wa Chadema, basi watoe tamko la hadhara kumwambia Dr. Nchimbi sisi Polisi hatufanyi kazi kwa maagizo ya CCM, na hatutawaachia viongozi wa Chadema.
Na upande wa pili, viongozi wa Chadema wasikubali hizi drama za kipumbavu zinazofanywa na Polisi. Wadai haki yao ya kupelekwa mahakamani kwa kosa walilokamatiwa. Wasipopelekwa, au wakipelekwa wakashinda hiyo kesi, wawafungulie mashitaka binafsi ya madai viongozi wa Polisi wa juu na waliohusika na ujinga huu.
Ifikie mahali Polisi walipe kutokana na ukosefu wa akili wanaoufanya mara kwa mara. Tumechoka sana na hili genge la wajikombaji wa CCM wanaojiita Polisi.
Pia soma: Kuelekea 2025 - Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi aiagiza Serikali kuwaachia Viongozi wa CHADEMA