Kama Rasimu itapitishwa bungeni na wabunge wa chama kimoja!

Kama Rasimu itapitishwa bungeni na wabunge wa chama kimoja!

ansebaluu

Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
21
Reaction score
9
Hivi karibuni tumeona mambo yaliyotokea bungeni kwa Naibu spika kuminya haki za wabunge wa upinzani. Kitendo kilichopelekea wabungea hao kutoka nje na hivyo kuacha mchakato wa maswala ya rasimu kuongelewa na wabunge wa chama tawala tu. na wabunge wawili wa upinzani waliobaki kwa sababu wanazozijua wao. Kitendo hiki si tu kinaminya demokrasia bali kinatupeleka kusiko. Nako ni kwenye uwezekano wa kuwa na mgogoro wa katiba mbeleni.

Mimi kama Mtanzania nayependa nchi yangu nasema sikubaliani na hili jambo katu!

kwa sababu hii sasa maamuzi yangu endapo rasimu itapigiwa kura na kupitishwa na wabunge wachama kimoja. NASEMA HAKIKA SITAPIGA KURA YA KUIKUBALI. HUU ni uamuzi wangu tu kama mzalendo.
 
Maamuzi ni yako mkuu hulazimishwi na mtu kuikubali katiba. Isitoshe katiba si ya vyama vya siasa peke yake, kuna mambo mengine muhimu ambayo sisi wengine tunayaangalia ukiacha hizo siasa zenu za CCM na Chadema.
 
Kama ni hivyo basi kwa pamoja tunasema hatukuabali. Hebu angalia. Kamanda lema alisema hakuna dhambi kama uoga je watz mpoo. Km nyie ni waoga basi mnadhambi kama hamtaki dhambi basi tuna sema hatukubali

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom