Kama si Mbwa kusababisha goli, United ingeshuka daraja ligi ya 1987

Rahma Salum

Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
30
Reaction score
59
Pengine ni kitu cha kustajabisha masikioni mwako kufahamu mbwa kusababisha goli katika mchezo wa mpira wa miguu. Nafahamu upo na shauku na maswali mengi juu ya jambo hili la kushangaza, soma mkasa huu uliowavutia wengi zaidi miaka 34 iliyopita.

Timu inayozungumziwa hapa ni Torquay United, si United inayotokea Manchester. Ikiwa inaongozwa kwa mabao 2-0 katika kipindi cha kwanza cha mchezo uliokuwa muhimu kwa timu, kwani wangefungwa klabu hiyo ingeshuka daraja. United walihitaji angalau sare tu ili kusalia juu.

Wakiwa wanaongozwa kwa bao 2 zinazo tishia na kupoteza matumaini kwa timu, Torquay United ilihitaji kuokoa kitu kutoka kwenye mchezo huo ikiwa walikusudia kukaa juu na sio kuwa timu ya kwanza kushushwa ligi ya soka mwaka 1987.

Mchezo ukiwa katika kipindi cha pili Jim McNichol alirudisha goli la 1 kupitia free-kick, hapo sasa tumaini likaanza kuonekana. Lakini kilichotokea baadaye ni kitu ambacho hakuna mtu angeweza kutabiri. Mfungaji McNichol alikimbilia mpira uliokuwa unakaribia kutoka nje, ghafla alitokea mbwa wa askari na kumng’ata mlinzi (defender) huyo.

Inavyoonekana, mbwa huyo aitwaye Bryn alidhani kwamba mlinzi huyo alikuwa akikimbia kumshambulia muangalizi wake, na hivyo alirarua miguu ya McNichol kwa meno yake. Beki huyo alikuwa chini kwa dakika 5, na dakika 5 ziliongezwa kwenye mechi hiyo iliyokuwa ikielekea ukingoni kama muda ambao unafidia majeruhi yaliyotokea.

Dakika 5 zilizoongezwa zikawa kama bahati kwa United, Paul Dobson alifunga goli la kusawazisha katika dakika ya mwisho ya muda ulioongezwa, ambayo ilitosha kuweka Torquay United kubaki juu. Torquay United inacheza katika ligi ya Taifa ya Uingereza (England National league).

Jim McNichol alishonwa nyuzi 17 kwenye jeraha alilopata.
 
Umetumia united ili kuvuta wasomaji hongera kwa ubunifu

Ila mbona hujasema hiyo ilikuwa ligi ya wapi?
 
Nimekuja mbio nikijua ni united ya Olesendeka!
 
Rahma Salum Mwanachuo..?
Karibu sana JF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…