Mkuu JokaKuu,
Hapo umenena, sioni sababu ya mjadala kuhamia kwenye mashambulizi dhidi ya Nyerere, litakuwa jambo jema kama watu watafahamishwa kuhusu makuu aloyatenda Mzee Jumbe. Yaliyomkuta Mzee Jumbe hayakusababishwa na Nyerere pekee, sidhani kama alikuwa na uwezo huo, bali watu kama kina Seif na kiu yao ya kuongozi visiwa hivyo, ni wazi walitumia mwanya ulojitokeza kummaliza Mzee Jumbe wakitambuia udhaifu wa Mwalimu linapokuja suala la Muungano.
Bado narudia kila kiongozi anapita katika wakati wake, huongoza kulingana na mazingira ya wakati huo, hivyo uongozi wake huwa na matokeo hasi na chanya, hauwezi asilani ukawa na mazuri matupu. Hata Amini pamoja na kuonekana kuwa kiongozi dhalimu bado kwa Waganda yapo mazuri alowafanyia na wanamkumbuka kwa hayo pia.
Mzee Jumbe kafanya mengi kwenye ujenzi wa demokrasia visiwani humo, hilo halina ubishi na anayepinga ana lake jambo.